Mahari hutolewa ili angalau kuwafurahisha(kuwafariji) wazazi kwa kuamini kuwa angalau watakuwa wamepunguza gharama walizopata wakati wakimkuza mtoto wao tangu utotoni na pengine gharama ya elimu yake.
Kwa huku Tanzania na nchi nyingine nyingi wanaume ndio huwatolea mwanamke mahari, ila nchini India wanawake ndio huwatolea wanaume mahari.
Hii kitu ni upuuzi tu kwa nini na mwanaume asitolewe mahari kwani yeye hajalelewa? unakuta unatoa mahari kubwa kwa kuoa kicheche bora hii kitu ingetolewa kwa wasichana walioolewa wakiwa bikra na pia isipangwe iwe kama shukrani tu na sio lazima maana sioni logic ya hiki kitu kabisa coz kiuhalisia huwezi kumlipia mtu gharama za matunzo hata kama mtoto wa miaka 10 kwa sababu hakuna record ya gharama pili kuna gharama ambazo none monetary costs hizo nazo sijui zinalipwaje.So swala la mahari ni moja ya kitu kinachofanya wazungu na jamii zilizoendelea kutuona tunaishi maisha ya kigorilla.