wananchi tunatakiwa tulaani kwa nguvu zetu zote na tupinge kwa nguvu zetu zote kwa vyama vya siasa kuanzisha vikundi vya jeshi au ulinzi kama wao wanavyoweza kuita. mtu yeyote au kikundi chochote kinachoanzisha kikundi cha jeshi katika siasa au dini huyo/hicho ndicho adui mkubwa wa amani yetu. hakuna sehemu vikundi hivi vimeleta maendeleo bali kuwafanya wananchi wakimbizi, wengine kuuawa na wengine kupata vilema vya maisha, wengi wamepoteza mwelekeo wa maisha. watu wanapokuwa wanatafuta madaraka watatumia njia yoyote na wakiona wameshindwa wanakimbialia msituni ili ama wachukue kwa nguvu au waitwe kwa mazungumzo na wapewe madaraka. bado nasisitiza katiba mpya ipunguze kwa kiasi kikubwa nafasi za uteuzi wa raisi hasa kuongoza taasisi na mashirika ziwe za kuwania kwa ushindani wa sifa. nafasi za kuteua zibaki chache sana hasa za mawazili tutapunguza chokochoko katika siasa