Miezi kadhaa iliyopita tulitaarifiwa kuwa kutakuwa na mvua zitakazonyesha zaidi ya kiwango maeneo ya Kanda ya Ziwa kuanzia Oktoba. Mpaka leo mvua zaidi ya kiwango haijanyesha licha ya manyunyu tunyoyaona katika tarehe za katikati ya Novemba. Hakuna aliyekwishapanda na sasa hivi tungekuwa kwenye kipindi cha kupalilia. Tupeni taarifa ya uhakika ya hali ya hewa kuelekea Desemba mpaka Februari mwakani.