Sonona
1. Msione wajifia, vijana naso wakubwa
Mawazo nawaambia, akili ndio hukabwa
Fuadi zinaumia, mwili nao dabwa dabwa
Sonona gonjwa hatari
2. Akili inapofeli, mauti yatawasili
Hutaona afadhali, ila ni ubahaluli
Jambo la kutaamuli, vigumu kulikabili
Sonona gonjwa hatari
3. Kazi hutaitamani, itakujaa simanzi
Hutakuwa na amani, kila wakati majonzi
Joto lililo kichwani, halipoagi kwa minzi
Sonona gonjwa hatari
Abuuabdillah
0744 883 353