Ila sijaona walipokutukana, sana sana nimeona mmoja ametania unaleta utitiri akimaanisha ID yako, mwingine kasema panya lakini si kwa kukuita wewe utitiri au panya. Na jinsi walivyoandika ni kama wanafanya jokes tu. Sasa matusi ya nguoni sioni kama wamekutukana sasa iweje wewe utumie matusi makubwa hivyo kwa mambo madogo tu. Sasa hapa ni jukwaa la matangazo, ukienda kule jukwaa la Siasa utahimili kweli? Nakushauri kabla hujajibu utulie upate kwanza busara. Ni ushauri tu usije na mimi ukaanza kuniporomoshea.