Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,067
- 34,829
Halo MziziMkavu, kumbe wewe mkali kwenye mistar! Naikopi hii nikafundishie somo la ushairi! kwa hisani ya MziziMkavuSISIMIZI!
- Si mkubwa kama temba lakini ana udhia
Ni mdogo mwenye mambo Kidudu kisosikia
Ficha hata kwenye tumbo Ujue ataingi
Sisimizi kanishinda Sijui nifiche wapi.- Atambalia vitamu Vikali avichukia
Vya nje na ndani hamu Vyote anavifatia
Huwa tena sina hamu Ni kheri kumuachia
Sisimizi ana ila Kutambalia vya watu.- Sisimizi hana kimo Angepigwa akalia
Angelifundishwa somo Milele angetulia
Bali hesabuni hamo Kupigwa ataonewa
Sina haja kushindana Kuteta na sisimizi.- Sisimizi hatosheki Kwa vyote vilosalia
Ameshawekewa keki Yenye pira maziwa
Bali yeye haridhiki Vyetu kuja tambalia
Sisimizi wacha inda Vya watu kutambalia.- Sijui nifiche wapi Ashidwe visogelea
Tena hutambua vipi kama tunamtambua
Huvizonga haogopi Na wenzake huwambia
Sisimizi kanishinda Sijui nifiche wapi.- Niseme niweke sumu Hasara nitajitia
Tajikosesha vitamu Sisimizi kuchelea
Na yeye akifahamu Chakula hatokijia
Nipeni tiba ya dawa Nimuweze sisimizi.- Wale wafukuzao dawa Vidudu nawaambia
Mende,kunguni na chawa Hao hawana udhia
Kuliko vidudu hawa Vyakula kutufujia
Sisimizi wacha inda Vyakula kutambulia.