Je, unataka kuwa masikini? Je, unataka kuwa fukara?
Basi hapa umepata suluhisho. Cha kufanya fuata haya maelekezo na utakua masikini na fukara moja kwa moja
1. Kuwa mvivu. Uvivu ni tiketi moja kati ya tiketi za umasikini. Ninaposema uvivu, naongelea kwa ujumla. Kuna uvivu wa kufikiri na uvivu wa kutenda wewe kuwa mvivu wa aina zote. Hakika umasikini utakufika. Na hata kama wewe ni masikini na unataka kuendelea na umasikini wako, endelea tu kuwa mvivu wala huhitaji kitu kingine.
2. Kuwa mtu wa kutoweka akiba. Chochote unachokipata kitumie. Usiwaze kuhusu kesho. Hakika utafanikiwa kuwa masikini. Na hata kama wewe ni masikini, hakikisha kuwa unatumia chote unachokipata. Usibakishe kitu
3. Fanya kazi au biashara zisizo na maslahi. Endelea tu kufanya kazi inayokupa nauli tu ya kukupeleka unapofanya kazi. Hiyo kazi usiiche maana ndio tiketi ya kuendelea kuwa masikini
4. Ishi bila malengo. Hapa utakua umeshafika stand kabisa kupanda gari ya umasikini. Wala usijipangie ya mwaka au miaka mitano ijayo
5. Endelea kutegemea vya watu wengine. Hiki ndo cheti cha umasikini. Wala usitamani kuwa na vyako.
Kwa leo naishia hapa. Nitaendelea hapo baadae kupeana tips za kuwa masikini. Wala msijari, tuko pamoja