Siri: Mapenzi nayapata na sipigwi mizinga

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,379
Kuna wanaume wengi sana wanaamini ya kwamba pesa ndio kila kitu katika mapenzi, Hii hali imekua tofauti sana kwangu na ni mara nyingi marafiki na ndugu zangu nimekuwa nnikiwaacha midomo wazi pale nnapowaambia maisha yangu ya kimapenzi na wanawake hayanaga mizinga.

Tangu sekondari, chuoni na mpaka sasa nikiwa Muhasibu fulltime na blogger part time nakiri ya kwamba wanawake niliokuwa nao kwenye mahusiano hakuna hata mmoja ambae ana itikadi za kuniona buzi na kunipiga mizinga isiyo na mbele wala nyuma,

Kwa nyakati chache tofauti tofauti nimejikuta nikiwa katika mahusiano na mabinti niliogundua mbeleni kwamba waliachwa kwa shutumaza kuwaomba sana hela ma ex-boyfreind wao,,, Lakini hali inakuwa tofauti sana kwangu, baadhi ya hao waliowaacha huwa tunajuana so ninapowaambia kwamba kwangu mambo ni mazuri huwa nawachanganya sana kiasi kwamba wengine wanadhani natumia kizizi.

Pia kuna mara nyingine kwa sababu kadha na kadha naamua kuachana kiroho safi kabisa na girlfriend wangu, Watu wengine ambao wanaanzisha mahusiano na hao niliowaacha napataga stori zao jinsi wanvyolalamika juu ya kupigwa mizinga, washkaji wawili wamewahi kunifata serous na wakaniuliza mbona mimi hawakuwa wakinifanyia kama wanavyowafanyia wao ila nilibaki nacheka tuπŸ™‚πŸ™‚

Nachoweza kusema ni kwamba mwanamke ataku-treat kulingana na wewe imani zako na mienendo yako. kama wewe ulimfata kwa vihela basi anyeye penzi lake kwako litapumulia wallet yako...kama wewe ulimfata wewe kama wewe na chemistry zenu zikafanana basi jua tu ya kwamba mnaendana na hana haja ya kutafuna wallet yako.

Mapenzi yaliumbwa kwa wapendanao, mapenzi inabidi yawe natural....Usishangae hata kidogo umemwacha demu kisa anakuchuna mshahara wako wote ila akapata mwengine ambae hamchuni hata kidogo.....Love is natural guys na pindi mnapoingiza pesa tu mnapata cha kufosi na sio kinachokutaka.
 
"Hakuna hata mmoja ambayeana itikadi za kuniona buzi na kunipiga mizinga isiyo na mbele wala nyuma" haya maneno yako kwenye insha yako[emoji23]
 
Umebalehe lini???
 
Mwanaume machine jua kuna wengine wanahudumia na pole Kwa kupoteza nguvu zako
 
"Hakuna hata mmoja ambayeana itikadi za kuniona buzi na kunipiga mizinga isiyo na mbele wala nyuma" haya maneno yako kwenye insha yako[emoji23]
Kwa maana kama ni mizinga bado anapigwa kwa vile karidhika nayo anasema kwa kuitetea kuwa si mizinga isiyo na mbele wala nyuma!! Good observation!!
 
" Natambaaaa " by aslay. [emoji23] [emoji91] [emoji378] [emoji13]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…