IJUE #KWANZAA, SIKUKUU YA WAAFRIKA NA UAFRIKA
Baada ya Ukoloni Waafrika tulivurugwa na tamaduni mpya na za kigeni na kutupa kabisa mila na desturi zetu. Tumepokea majina ya kigeni, mila za kigeni, vyakula vya kigeni mpaka dini za kigeni.
Hii imesababisha waafrika kukosa vitu vya kujivunia. Tofauti na wenzetu kama Waasia, Warabu n.k Waafrika tumepoteza hata sikukuu zetu, sikukuu zote tunazoadhimisha kwenye karenda zetu ni sikukuu haidha za kisiasa au kimagharibi na Mashariki ya Kati.
Miaka ya 1960 nchini Marekani Professor wa African Studies na Mwanaharakati Mweusi Ronald McKinley Everett ambaye baadaye alijiita Maulana Karenga alizindua Sikukuu aliyoipa Jina la #KWANZAA. Neno kwanza limetokana na neno la Kiswahili #Kwanza na dhana nyuma yake ikiwa ni Sherehe ya Matunda ya Kwanza.
Karenga anasema Kwanzaa ni sikukuu ya kuazimisha siku ya utamaduni wa mtu mweusi, umajinuni wa kiafrika hasa kwa watu weusi waishio Marekani (Diasporas). Sikukuu hii uazimishwa kwa wiki moja kuanzia 26 ya Dec mpaka 1 Jan kila mwaka.
#Kwanzaa ni mapinduzi ya kitamaduni yanayolenga kumpa mtu mweusi Utambulisho, kutoa Dira na Kusudio (Purpose) na muhimu zaidi kueneza kwa vizazi vya kesho
Je ni Kweli #Kwanzaa ni Mbadala wa Christmas?
Karenga Maulana anasema, ni kweli alilenga #Kwanzaa kuwa mbadala wa Christmas, anabainisha kwamba "Christmas ni sikukuu ya Wazungu na kwamba waafrika wanatakiwa kujitenga nayo"
Lakini baada ya Sikukuu hii kupata muitikio mkubwa huko Marekani, Karenga aliregeza msimamo wake na kusema kwamba "sio LAZIMA Sikukuu hii isherekewe na watu wasio na dini au ambao hawapendi Christmas, “Kwanzaa sio Sikukuu ya Kidini ni Sherehe ya Kiutamaduni, hata kama unapenda Ukirsto wako ni ruksa kusherekea Kwanzaa, #Kwanzaa ni Sikukuu ya Familia, Jamii na Utamaduni”
Nguzo Saba Za #Kwanzaa
Kwanzaa ina nguzo Kuu Saba ambazo zinaipa maana pana zaidi Sikukuu hii.
1. Umoja (Unity)- Kujenga umoja baina ya Familia, Jamii, Taifa na Ubinadamu
2. Kujichagulia (Self Determination)- Kujitambua kwa kurejea asili yetu na kuzungumza kwa ajili yetu.
3. Ujima (Communal)- Kufanya kazi na kuwajibika pamoja kama Jamii
4. Ujamaa (Collective Economics)- Kujitegemea kiuchumi kwa kuanzisha biashara zetu na kutengeneza ukwasi kwa ajili yetu.
5. Nia (Purpose)- Kuwa na nia pana yenye kujenga jamii yenye utajiri wa kiutamaduni na kujitambua.
6. Kuumba (Creation) - Kufanya kwa kadri ya uwezo, kubuni kwa lengo la kujenga jamii njema yenye urithi wenye manufaa.
7. Imani (Faith)- Kuamini toka mioyoni mwetu, kwenye watu wetu, wazazi wetu, waalimu wetu, viongozi wetu, kwa pamoja na ushindi wetu.
Jinsi ya Kusherekea #Kwanzaa
Kwanzaa inasherekewa kwa uwepo wa Mkeka, Kinara (Candle holder), Mishumaa Saba (Kuwakilisha Nguzo Saba), Mazao (Kuwakilisha Mavuno ya Kwanza, Muhindi (Ishara ya Mapambo na Mlo), Kikombe Cha Umoja kwa ajili ya Kukumbuka na Kutoa Shukrani kwa Mababu Zetu, na Mashujaa wa Africa Pamoja na Zawadi Mbalimbali.
Vitu vingine ni kama Kitambaa cha Nguzo Saba, Bendera ya Rangi Nyeusi, Nyekundu na Kijani pamoja na vitabu na Majarida mbalimbali ya Kiafrika na Kazi za mikono kwa ajili ya kuwakilisha Utambulisho, Thamani, Mila na desturi ya mtu mweusi. Salamu maalumu ya hii siku ni #HabariGani
Familia husherekea Kwanzaa kwa Kupamba nyumba zao kwa vitenge, kuvaa nguo za kitamaduni, na mapambo mbalimbali. Watoto hupewa mafunzo mbalimbali yenye urithi wa kiafrika. Kikombe cha Umoja upitishwa kwa kila mtu kwa ajili ya kutia baraka. Alafu kuna ngoma, nyimbo na michezo mbalimbali ya Kiafrika alafu inafuata Karamu kubwa ya milo na vinywaji.
Hii ndio sikukuu ya #Kwanzaa kama inaleta maana kwako naomba nikutakie #Kwanzaa Njema
-Charles B
26th Dec 2018