Sikuja Yanga Kuifunga Simba -Maximo

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
Siku chache baada ya kuanza kuifundisha timu hiyo, Maximo amesema hakuja kumfunga mtani wake wa jadi Simba kwa kuwa hayo si mafanikio timu hiyo inayohitaji

Nipashe Julai 5
 
Aanze kujitetea mapema kabisa
 
Hawa wanawaza magari, wengine wanawaza Farasi"
 
Maximo ana tabia ya kuijenga timu taratibu kwa malengo ya muda mrefu tofauti na matarajio ya jamaa zangu ya BRN, mkipigwa mechi 4 au 5 mfululizo mtaanza kuandamana
 
Dunia nzima timu hukamia mashindano, hazikamii mechi. Pengine ni falsafa ngumu kwa wasioelewa hilo, wakiwamo wataomshangaa Maximo kwa kauli yake hiyo. Maana yeke sio kwamba timu fulani iko tayari kufungwa na mpinzani wake mkuu, lakini ni bora kufungwa na mpinzani huyo na kutwaa ubingwa kuliko kukosa ubingwa licha ya kumfunga mpinzani huyo.
 
Siku chache baada ya kuanza kuifundisha timu hiyo, Maximo amesema hakuja kumfunga mtani wake wa jadi Simba kwa kuwa hayo si mafanikio timu hiyo inayohitaji

Nipashe Julai 5

Maximo inaelekwa haijui nini kitakachomtoa Yanga kabla ya mkataba kuisha.
 
Nimemuelewa amekuja kuifundisha yanga iwe na uwezo kimataifa na si kisimba na kiazam etc
 
anachoongea maximo ndio ambacho kocha yeyote mwenye busara anatakiwa aseme. Kuna maana gani kuwafunga simba kisha ubingwa kuukosa? Lakini kuna maana kubwa kuwafunga simba na kuchukua ubingwa!
 
Huyu mzee atakuja kuchemsha vibaya sana. Ataondoka kwa aibu
 
Maximo ana tabia ya kuijenga timu taratibu kwa malengo ya muda mrefu tofauti na matarajio ya jamaa zangu ya BRN, mkipigwa mechi 4 au 5 mfululizo mtaanza kuandamana

ni kweli tatizo wapenzi uvumilivu zero, tena hata mchukue ubingwa, mkifuyngwa na YANGA Maximo hana max tena
 
kauli ya kiungwana sana ni nadra kuisikia
 
Huyu mzee atakuja kuchemsha vibaya sana. Ataondoka kwa aibu

namjua ni mechanics coach sio technical, ni kama alivyo morinyo tu hivyo ni lazima apate majembe sana aweze kushinda
 
Tanzania tuna safari ndefu sana ya kufikia mafanikio ya soka la kisasa, mm binafsi sijawahi kusikia timu yoyote barani ulaya inamuajili kocha kwa lengo la kuifunga timu pinzani, sidhani kama abrahimovic alimuajili morinho pale chelsea kwa lengo la kuja kuifunga arsenal, ila ninachokiamin mm boss yeyote wa timu humuajili kocha kwa lengo la timu yake ichukue makombe mbalimbali ila kwa tz ni tofauti kabisa ili uonekane kocha bora basi kocha wa yanga aifunge simba au kocha wa simba aifunge yanga hata kama timu yake haijachukua ubingwa au kuwa katika nafasi tatu za juu....tanzania ni nchi ya tofauti sana na nchi nyingine.
 
Ni kweli Maximo amekuja Yanga kufundisha soka, hakuja kuifunga Simba. Simba ataifunga kama timu nyingine pinzani itakayokutana na Yanga uwanjani.
 
Ki ukweli timu zetu za simba na yanga hazina muamana! Mzee wetu Maximo kukubali kufundisha mojawapo ya timu hizo ni kama kaja kuharibu CV yake! Huyu safari hii atarudi Brazil akiwa hana hamu tena na TZ..! tusuburi!!
 
binadamu wepesi kusahau
 
Yanga na Simba zipo ovyo, mfano Kibadeni Aliifunga Yanga Mfulilizo lakini alikuja kufukuzwa kama mbwa, Raul Shungu aliifunga Simba Mfulilizo naye alikuja kutumuliwa, Simba na Yanga zinawatu wake wakisema unakaa sawa wakikuchoka tu basi unaondoka. Mfano wa kocha Siang'a au Nzoisaba mafanikio yao yalivyokuwa lakini wenye timu walipowachoka wakawatimua. Ata huyo Maximo aifunge Simba kila mechi hatamsaidia mwenye timu akimchoka nje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…