kabiriga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 1,163
- 1,213
Miaka mitano iliyopita nilikuwa na mahusiano na binti mmoja!katika utafutaji na hali ya maisha niliamua kwenda kujiendeleza kimasomo,sikumuaga ingawa baadae tuliendelea kuwasiliana kwa njia ya simu.Kwa muda wote wa masomo yangu (miaka 3) sikurudi nyumbani baada ya kuhitimu masomo yangu nilienda kutafuta kazi mkoa mwingine yaani mkoa tofauti na ule nilikokuwa nasoma nikapata kibarua na kufanya kazi huko kwa miaka miwili.Baada ya kibarua changu kukoma nikarudi nyumbani ndipo nikakutana na huyo bibie kwa mara nyingine tena,alipo pata habari kuwa nimerudi alinipigia simu akiomba tukutane.tukakutana kwenye mgahawa mmoja katikati ya maongezi yetu aliniuliza kama mapenzi yetu yanaendelea au yalikoma? mimi nili mjibu kuwa ni muda tumekuwa hatupo pamoja kwa hiyo si busara kuendeleza mapenzi yetu na kibaya zaidi nilishakuwa na mtu mwingine.ndipo alipo toa kauli hii tata ya "MIMI SIKUBALI nilisha kupenda wewe na nitafanya lolote liwalo maadamu niwe na wewe" kisha akaondoka.Natafakari sana kauli yake na nimekosa la kufanya ndipo nikawageukieni wanajamvi .ushauri tafadhali