Siku Yaja

Acha Uvivu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
524
Reaction score
131
Siku yaja na i karibu kufika. Ni siku ambayo yule anayekula kwa raha wakati huu kwa sababu ya kutaabika kwa watu waliyowengi ataelewa kuwa ni utulivu wa hawa waliyo kwenye tabu unamfanya ajisikie kula raha za dunia. Huo ni wakati ambao yule aliyezoea tabu hataogopa kufa ila aliye kwenye starehe atashiriki kuwaangamiza kwa mkono wa unyama hao aliyowaibia ili aweze kula raha zake zaidi.

Katika mazingira ambayo anawatesa kwa siri siri na kusababisha vifo kwa njia zisizo za wazi kama kutowapatia waja wa Mungu vifaa vya kutoa Oxygen wanaposhindwa kupumua mahospitalini na hatimaye kupoteza maisha, lakini ambao wangepona kwa uwepo wa hizo huduma za msingi.

Siku hiyo ambayo i karibu, mtu huyo mtesi atabadili mbinu ya kuwaangamiza anaowaibia na kuwasababishia tabu wakati huu. Badala ya kuwaua kwa kupata magonjwa ya kuhara kunakosabishwa na ukosefu wa huduma ya maji safi na salama (kipindu pindu) na kuua kwa kutumia kemikali za migodini na viwandani zinazotiririshwa kuingia vyanzo vya maji, badala yake siku hiyo ikifika atamwangamiza mlala hoi aliye mnyonya kwa muda mrefu akimwangalia husoni wakati anauachia mtutu. Wakati huo waja, muuaji hatamfunga kitambaa anayeuliwa/kuteswa bali atamtazama uso kwa uso na kuuambia mtutu nenda. Dalili zaonekana na hayana budi kutokea.

Ni wakati huo ambao kila mkazi atakayekuwepo siku hiyo na aliyeishi kwa tabu atapata kutambua kuwa ili nchi iendelee haihitaji MaliAsili bali MaliAkili. Na kwamba kila mmoja atajifunza kuwa anapoahidiwa kama mtoto mdogo kuwa nyamaza kulia, nitakuletea pipi lakini kumbe hailetwi. Ndipo huyu aliyedanganywa muda mrefu atakosa uvumilivu kwa kutambua kuwa anayesema atamletea pipi na ambayo hata kwa udogo wake bado hailetwi, atavamia sehemu zote ambazo mtoa ahadi anapata mali kwa ajili ya kujineemesha mwenyewe. Na tayari imeanza kuönekana, haya niyanenayo hayana budi kutokea. Lakini wakati huo vyombo vya habari havitakimbilia kusini bali vitahangaika huku na huku maana hamna ambako hakutakuwa na habari ya kuvutia.

Pande zote za nchi zitatikisika, linakochomoza jua mpaka linakozama, vinakoanzia vyanzo vingi vya maji mpaka vinakoishia walala hoi bila kushawishika kila mmoja atakuwa kiongozi wa yeye kwenda kumkabili anayewasababishia tabu, aliyewadanganya kwa pipi muda mrefu na maneno matamu yaliyojaa harufu ya waridi, bila kuamrishwa na yeyote isipokuwa njaa na ugumu wa maisha wote watasimama kumkabili yule mwovu na mtesi wao ambaye anatambua kuwa mchezo wa ahadi ya pipi umebumbuluka, sasa akija kwa kutisha na kutesa kwa njia ya kutoa meno na macho usiku na kuwafunga vitambaa.

Siku inakuja kwa mwendo wa kasi sana, ambayo itakuwa ni kuinama na kuinuka na wote kutambua kuwa ili nchi iendelee haihitaji MaliAsili chini ya TAPANA bali MaliAkili chini ya mkono wa Mola. Ni wakati ambao wote watatambua kuwa chaguo la mungu lililopo ni la mungu wa herufi ndogo, sio Mungu wa herufi kubwa na kwamba wa herufi ndogo anategemea sana MaliAsili (vitu vya anasa) na sio MaliAkili (hekima na Maarifa). Haya yote hayana budi kutokea, naam, anena mleta mada.

Mleta mada akaguswa na mwenendo wa danadana na chenga tu bila kufunga magoli ktk mstakabali wa taifa la walala hoi na kuhitimisha kuwa siku yaja na ikaribu kutimia, kwamba Libya ni nchi ambayo kwa jiografia iko jangwani lakini si MaliAsili bali ni MaliAkili imeweza kuwa na maendeleo. Lakini nchi ambayo iko hatarini inajivunia MaliAsili na sio MaliAkili kwa maana elimu ambayo ndo msingi wa kuwa na MaliAkili imeangamizwa na kila mmoja anawaza MaliAsili (wanafunzi kuruhusu mimba kwa viherehere vya kupata MaliAsili). Lakini wote watafunuliwa katika siku hiyo na kusema adui wetu ni mmoja.
Anena mleta mada.

PAGE 1.
 
Nimefungua kwa kasi nikijua unaongelea siku ile ambayo kila ulimi utakiri ya kuwa BWANA WA MAJESHI anasitahiri kuabudiwa, hata na wale ambao wanadai kuwa hayupo, siku hiyo watakiri lakini kwa kuchelewa.
 
Nimefungua kwa kasi nikijua unaongelea siku ile ambayo kila ulimi utakiri ya kuwa BWANA WA MAJESHI anasitahiri kuabudiwa, hata na wale ambao wanadai kuwa hayupo, siku hiyo watakiri lakini kwa kuchelewa.

Mkuu hujajipanga nini, kwa nini usituke kwa kudhania siku ya kiama cha roho? Mada inazungumzia kiama cha kimwili dhidi ya wanyonyaji waliojaa tamaa za kimwili. Maana wao wanajineemesha na maisha ya dunia wakati waliyowapa dhamana wanataabika na hata kuishi kwa wasiwasi ya kuteswa na vyombo vyenye kujiita vya usalama vilivyopoteza majukumu halisi na kujiingiza ktk maslahi na kujidharirisha.

Kila palipo na mwana usalama mmoja kuna zaidi ya Watanzania elfu kumi wanataabika na kuomba kuthaminiwa siku moja. Wasipopata kuthaminiwa wataona bora kuweka maisha rehani.
 
Ulishajaribu kumtupia mbwa mwenye njaa mfupa wenye minofu, alafu ukajaribu kumyang'anya? Kuna kazi kubwa kwa siku hiyo unayosema. Kuwanyanganya ulaji, wallahi watatumia mbinu zote wasiachie. Wataiba, watanyang'anya, watatumia polisi, FFU, JWTZ, Tume ya uchaguzi, pesa za BOT na kila kinachowezekana mradi wasing'oke. Inategemea wapinzani wao wamejiandaaje kukabili mbinu hizo!!!
 

Uliyonena ndo waliyonayo pia, lakini kama umeielewa mada na unafuatilia na ukajionea hasira ya watanzania juu ya maisha wanayopitia jibu litakuwa wazi.
 
Naona umeanzisha thread ya kupatia hela ya supu kesho asubuhi. Njaa mbaya sana.
 
Siku ikaribu mno ila hatujui lini na wakati gani hii hasira ya wananchi si ya kawaida sasa hivi wamejizira na wameshachimba makaburi yao ili mradi warudishe heshima ya utu wao,haki yao ya kuishi kama wengine na haki ya kujitafutia kipato halali bila kuwekewa vizingiti hakika siku ya aja na ole wao watakaotaka kuzia siku na saa itakapofika
 
Naona umeanzisha thread ya kupatia hela ya supu kesho asubuhi. Njaa mbaya sana.

Km unaamini mtu anaweza kuleta mambo mazito kama haya ya ufunuo ili tu apate ya supu basi ni ishara kuwa nawe unatambua kuwa watanzania wanataabika na kwamba wako tayari kupokea chochote kwa riziki ya siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…