A Father
JF-Expert Member
- Nov 11, 2012
- 1,385
- 602
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014, KIDATO CHA NNE MWAKA 2014 NA JKT MWAKA 2015 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI
UTANGULIZI:
Jeshi la polisi Tanzania linawajulisha kwamba litaendesha mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi kwa miezi tisa (9) katika shule ya Polisi Tanzania ¡°Moshi¡± kuanzia tarehe 29/08/2015. Mafunzo hayo yatahusisha wahitimu wa vyuo vikuu, kidato cha sita (f6), kidato cha nne (f4) wote wa mwaka 2014. Aidha wahitimu wa Jeshi la kujenga Taifa wa mwaka 2015 watahusika pia.
Maelekezo Muhimu.
1. Waliochaguliwa watatakiwa kuripoti kwa makamanda wa Polisi wa Mikoa Tarehe 28/08/2015 kwa ajili ya maandalizi ya usafiri wa kwenda shule ya Polisi Tanzania tarehe 29/08/2015 kila mmoja atatakiwa kuwa na nauli ya kumwezesha kusafiri toka makao makuu ya mkoa anakoanzia kusafiri hadi shule ya Polisi Moshi na atarejeshewa nauli atakapofika chuoni baada ya kuwasilisha Tiketi ya safari. 2. Tarehe ya mwisho ya kuripoti chuoni ni tarehe 5/09/2015 na atakayeripoti baada ya hapo hatapokelewa.
3. Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na vitu vifuatavyo : a) Vyeti vyao vyote vya masomo (original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne, Sita na vyuo,
Vyeti halisi vya kuzaliwa (Original Birth certificates), Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
b) Mashuka mawili rangi ya Bluu bahari (light blue)
c) Chandarua chenye upana futi tatu
d) Nguo za michezo (Track suit nyeusi, Tshirt blue na Raba)
e) Pasi ya Mkaa.
f) Ndoo moja.
g) Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/= tsh)
h) Pesa kidogo ya kujikimu.
4. Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.