Mwanafalsafa Mmoja alishawahi kusema kua "UJINGA NI KUFANYA KITU HICHO HICHO KWA KUKIRUDIA RUDIA HUKU UKITEGEMEA KUNA WAKATI KITAKUJA KUTOA MATOKEO TOFAUTI NA UNAYOYAPATA MWANZO".
Sijadhamiria kukuita mjinga ila nahofia tu usije kuingia huko. Hii ni kama Mara ya tatu unalitangaza hili shamba. Kuendelea kurudia rudia thread ni ishara tosha kua halipati wateja!!
Na halipati wateja sababu ya hizo bei za tamaa. Sioni factors za kufanya shamba liuzwe Tshs 8,000,000/- kwa heka kwa hayo maeneo. Hata kama lina kisima hakifiki hiyo bei. Haieleweki ni zao gani litalimwa hapo kama shamba irudishe hiyo hela.
Na kama ni prime area kwa viwanja basi ungepimisha viwanja uviuze ijulikane moja.
Ukifuata huu ushauri utakufaa. Na ukiupuuza basi tukutegemee tena kukuona next time ukija na same tangazo,same price.