Dotto C. Rangimoto JF-Expert Member Joined Nov 22, 2012 Posts 1,985 Reaction score 1,286 Jan 3, 2016 #1 LEO NAVUNJA KIBUBU! 1 Leo navunja kibubu, pesa ninunue khanga, Apendeze mahabubu, kama binti wa kitanga Atokapo awe bubu, washindwe wano jigonga Mniache nayajenga, mkome kunita zoba. 2 Sasa navunja kibubu, nipate nunua kanga, Ale ashibe muhibu, kitoweo si mchunga, Usiku tule kababu, uji pilipilimanga, Mniache nayajenga, mkome kunita zoba. 3 Mimi navunja kibubu, nikagule kungumanga, Nimpatie tabibu, mafusho toka Umanga, Nimuenzi taratibu, niseme na zake nyonga Mniache nayajenga, mkome kunita zoba. 3 Mie navunja kibubu, habibi apate shanga, Mapambo yake dhahabu, vidoleni na kitanga, Sawa nipate adhabu, apendeze wangu ninga, Mniache nayajenga, mkome kunita zoba. 4 Njano navunja kibubu, lengo niweze kujenga, Nyumba isiwe na tabu, mahaba yatie nanga, Penzi lataka adabu, siwezi kulibananga, Mniache nayajenga, mkome kunita zoba Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5) 0784845394/0762845394 mzalendo.njano5 Morogoro Tanzania kwa mashairi mengine kama hayo waweza kujisomea katika blogu yangu, kwenye icon ya mashairi utabofya hapo kisha utayaona mashairi mengi nilitotunga SASA HAMSINI RASI, HAMSINI MAJINUNI. | Kisima Cha Jangwani.
LEO NAVUNJA KIBUBU! 1 Leo navunja kibubu, pesa ninunue khanga, Apendeze mahabubu, kama binti wa kitanga Atokapo awe bubu, washindwe wano jigonga Mniache nayajenga, mkome kunita zoba. 2 Sasa navunja kibubu, nipate nunua kanga, Ale ashibe muhibu, kitoweo si mchunga, Usiku tule kababu, uji pilipilimanga, Mniache nayajenga, mkome kunita zoba. 3 Mimi navunja kibubu, nikagule kungumanga, Nimpatie tabibu, mafusho toka Umanga, Nimuenzi taratibu, niseme na zake nyonga Mniache nayajenga, mkome kunita zoba. 3 Mie navunja kibubu, habibi apate shanga, Mapambo yake dhahabu, vidoleni na kitanga, Sawa nipate adhabu, apendeze wangu ninga, Mniache nayajenga, mkome kunita zoba. 4 Njano navunja kibubu, lengo niweze kujenga, Nyumba isiwe na tabu, mahaba yatie nanga, Penzi lataka adabu, siwezi kulibananga, Mniache nayajenga, mkome kunita zoba Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5) 0784845394/0762845394 mzalendo.njano5 Morogoro Tanzania kwa mashairi mengine kama hayo waweza kujisomea katika blogu yangu, kwenye icon ya mashairi utabofya hapo kisha utayaona mashairi mengi nilitotunga SASA HAMSINI RASI, HAMSINI MAJINUNI. | Kisima Cha Jangwani.
M MAMENGAZI JF-Expert Member Joined Dec 31, 2010 Posts 779 Reaction score 129 Jan 5, 2016 #2 shairi limenikosha, lazima watambue hayajengwi kwa tofali kama nyumba!!!
Mafikizolo JF-Expert Member Joined May 8, 2014 Posts 3,487 Reaction score 1,627 Jan 5, 2016 #3 Nifa haya njoo uvunje kibubu huku