Sikutambua
Member
- Nov 16, 2014
- 46
- 5
Naipongeza Serikali Yetu Sikivu Kwa Kutoa Ajira Za Walimu Na Pia Walimu Wapya Hongereni Sana. Jamani Kuna Baadhi Ya Sekta Hadi Mtu Analaani Kwa Nini Alisoma, Naomba Serikali Izifikirie Sekta Hizo Kama Kilimo, Mifugo Na Nyinginezo.
Hapana mtoa maada, sekta za Kilimo na Mifugo zimekuwa zinaajiri watu direct. Tatizo moja ninaloona kwa sekta hizo ni wahitimu kutaka kuwa mjini tuu, hebu fikiri wewe upo afisa kilimo Dar-Ilala (Town Centre) kweli hapo mtakuwa wangapi? Natambua wanahitajika kwa ushauri kwa wahitaji lakini si kwa wingi kama vijijini kwa wakulima na wafugaji!
Naomba Nikujulishe Kuwa Kuanzia Mwaka Jana Wizara Ya Kilimo Imesitisha Kuajiri Direct Badala Yake Walianzisha Utaratibu Wa Kuomba Na Kufanyiwa Usaili, Pamoja Na Hilo Bado Nafasi Wanazotangaza Ni Chache Ukilinganisha Na Idadi Ya Wahitimu Na Mahitaji Ya Wataalam Vijijini, Serikali Iliangalie Hili.Hapana mtoa maada, sekta za Kilimo na Mifugo zimekuwa zinaajiri watu direct. Tatizo moja ninaloona kwa sekta hizo ni wahitimu kutaka kuwa mjini tuu, hebu fikiri wewe upo afisa kilimo Dar-Ilala (Town Centre) kweli hapo mtakuwa wangapi? Natambua wanahitajika kwa ushauri kwa wahitaji lakini si kwa wingi kama vijijini kwa wakulima na wafugaji!
Upo sahihi kwa namna moja ila kiuharisia ndg ulaji kwa sekta zingne ni mgumu sio siri ata km wapo dar ila kumbka huku ndiko mipango mingi hufanywa, watu wanakaa huku kujua wap upepo unakovuma maana matangazo yanatolewa huku ya ajira lakn vjijin unakodai ajira ndiko zlipo hamna hata gazet atazipataje hizo ajira?
Naipongeza Serikali Yetu Sikivu Kwa Kutoa Ajira Za Walimu Na Pia Walimu Wapya Hongereni Sana. Jamani Kuna Baadhi Ya Sekta Hadi Mtu Analaani Kwa Nini Alisoma, Naomba Serikali Izifikirie Sekta Hizo Kama Kilimo, Mifugo Na Nyinginezo.
Na Tourism sector
Dada yetu Tamalisa kuna huu utaratibu wa watu kuelekea vyuoni kusomea chochote....yaani akiwa hana loop ni nini cha kufanya baada ya kutoka chuoni!
Kama unapenda utangazaji usisomee Udaktari kisa tu unafaulu Biology na Chemistry darasani. Somea utangazaji. Utafanya vizuri zaidi. Watu wengi waliofanikiwa duniani wamefanya vitu wanavyovipenda!
Kama umesomea fani usiyoipenda kisa tu umeambiwa ina kazi za haraka haraka au ina hela umepotea. Siku ukimaliza kusoma usipate kazi au ukapata kazi lakini isiwe na hela kama ulivyotarajia utapata fadhaa na huenda kuchukia wale waliokushauri!
Kama umesomea kitu usichokipenda achana nacho, fanya kile unachokipenda na kinachokupa amani. Kama umesomea Sheria wakati moyo wako upo kwenye biashara ni ngumu sana kufanikiwa kupitia sheria. Achana na sheria, fanya biashara.
Hilo ni kweli na hiyo ni mada nyingine kabisa ambayo kama ingeletwa hapa tungeijadili kivyake. Kwani mimi kuandika Tourism sector umewaza nini?
Mtu akisema alisomea kitu fulani kisha hana kazi ya kufanya mara nyingi nawaza mtu huyo hakuwa na plan wakati akisoma alichosoma!
Mark Zukerberg mmiliki wa mtandao wa Facebook alikuwa anasomea shahada ya Uhandisi wa Computer akakosana na mkufunzi wake.Kama ilivyo kwetu alilazimishwa kukariri "Laws" za Pysics na za kina Gallileo Gallilei wengineo, lakini Mark hakutaka kukariri vitu vya watu, alitaka kubuni vya kwake.
Alipoona hawaelewani na mwalimu akaacha shule akaenda kufanya kitu alichokipenda na leo amefanikiwa sana. Leo Mark yupo kwenye list ya matajiri 10 wa dunia.
Mwanamuziki wa Congo aitwae Antoine Christopher Agbepa Mumba maarufu kama "Koffi Olomide" alisomea shahada ya Uchumi. Akafanya kazi kidogo bank. Lakini akaona anafanya kitu asichokipenda, maana moyo wake wote ulikuwa kwenye muziki. Akaachana na bank akaingia kwenye muziki na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa....Yatosha kukuonesha kwamba ulipo moyo wa mtu ndipo hazina yake ilipo!
Elewa wizara ya kilimo inaajiri kwenye sekta zake kama utafiti na waalimu wa vyuo,hao wengine wanaajiriwa na halmashauri husika
Na Tourism sector
Naomba Nijibu Hili, Dunia Leo Imekuwa Kijiji Hivyo Unaweza Kuwa Kijijini Lakini Taarifa Ukazipata Hata Kwa Kupanda Juu Ya Mti Kutafuta Mtandao Wa Simu, Pia Wataalam Wote Wanafundishwa Kuishi Mahali Popote Pale Ambapo Kuna Makazi Ya Watu, Kwa Hiyo Anaekataa Kwenda Kijijini Ana Suala Lake Binafsi