VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Hatari sana
.....karibuni mwaka 1998 nilimsikia waziri mmoja akisema katiba ni nyaraka ya serikali haichezewi!.....nchi hii ina maigizo.Waswahili wengi!.Naiomba sana Serikali ya chama changu. Iheshimu suala hili nyeti la katiba mpya. Katiba ni moyo wa nchi. Si jambo la kuletewa mzaha na maigizo. Nimesikitishwa sana na nilichoshuhudia kuhusu nakala za Katiba Inayopendekezwa. Kimeniuma sana. Nimelia kuililia nchi yangu inayoelekea shimoni.
Nimeshuhudia nakala za katiba zikiwafikia wananchi. Nimeshuhudia wananchi wakisoma kwa zamu,kwa saa chache,halafu nakala hiyohiyo kuhamishwa kwenda nyumba nyingine. Nimeshuhudia Katiba Inayopendekezwa ikisomwa kama gazeti. Nikalia sana.
Nimesikitishwa na mtazamo wa Serikali kuwa wananchi wanatakiwa kuiona na kuisoma tu Katiba Inayopendekezwa. Si kuielewa ili kuchagua upande sahihi kwenye kura ya maoni. Huu ni mtazamo hasi na wenye ukakasi. Ni mtazamo wa kiutani,kisanii na kimaigizo. Katiba ni nyaraka ya kisheria. Hata wasomi wenyewe waweza kuisoma na wasielewe. Seuse wananchi wa kawaida?
Serikali,tafadhalini,muwe makini. Kucheza na Katiba ni kuchezea moyo wa Tanzania. Tujirekebishe na tustopishe hima!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
hii nchi inakosa mwelekeo kutokana na uwingi wa viongozi wasio na matamanio yakutatua hoja na kubaki ktk ulafi wa madaraka
so what? Soma katiba inayopendekezwa sura ya nne, ibara ya 28-31 utaona inavyozungumzia mambo mbalimbali ya maadili na miiko ya uongozi, hivyo katiba hii ndo itakayotatua matatizo haya yote!!
Mkuu mbona nyie watu wa Lumumba swala la zitto mnalia Sana lakini hatuoni hata kada mmoja akitoa mwaliko Kama ilivyokuwa kwa akina Juliana shonza?
Wananchi hawatakiwi kuielewa. We unadhani wakiielewa wataipigia kura ya ndiyo? Kinachofanyika ni maigizo ya kuwaridhisha waangalizi wa kimataifa. Wananchi wengi hata kutafsiri biblia (msahafu) hawawezi sembuse lugha ya kisheria. Watawala wanajua walichokusudia hivyo wako tayari ipite hata kwa mtutu wa bunduki.
Naiomba sana Serikali ya chama changu. Iheshimu suala hili nyeti la katiba mpya. Katiba ni moyo wa nchi. Si jambo la kuletewa mzaha na maigizo. Nimesikitishwa sana na nilichoshuhudia kuhusu nakala za Katiba Inayopendekezwa. Kimeniuma sana. Nimelia kuililia nchi yangu inayoelekea shimoni.
Nimeshuhudia nakala za katiba zikiwafikia wananchi. Nimeshuhudia wananchi wakisoma kwa zamu,kwa saa chache,halafu nakala hiyohiyo kuhamishwa kwenda nyumba nyingine. Nimeshuhudia Katiba Inayopendekezwa ikisomwa kama gazeti. Nikalia sana.
Nimesikitishwa na mtazamo wa Serikali kuwa wananchi wanatakiwa kuiona na kuisoma tu Katiba Inayopendekezwa. Si kuielewa ili kuchagua upande sahihi kwenye kura ya maoni. Huu ni mtazamo hasi na wenye ukakasi. Ni mtazamo wa kiutani,kisanii na kimaigizo. Katiba ni nyaraka ya kisheria. Hata wasomi wenyewe waweza kuisoma na wasielewe. Seuse wananchi wa kawaida?
Serikali,tafadhalini,muwe makini. Kucheza na Katiba ni kuchezea moyo wa Tanzania. Tujirekebishe na tustopishe hima!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
hii nchi inakosa mwelekeo kutokana na uwingi wa viongozi wasio na matamanio yakutatua hoja na kubaki ktk ulafi wa madaraka
Mapambano Yetu! Wewe naamini ni kati ya watu wachache wenye maoni hasi na hatima ya nchi yako. Hivi kweli unaweza kulinganisha maisha yako na maigizo? Usiwatukane Watanzania nakuwafananisha na kuwaita kwamba wao ni miongoni mwaWananchi wengi ambao hata kutafsiri biblia (msahafu) hawawezi. Kwanini unawalazimisha kuwa hawawezi kuelewa? Hayo ni matusi kwa wananchi na dharau kubwa sana.
Waheshimu Watanzania wao ni wazalendo kwa nchi yao ndiyo maana wamnasema "KWA KUWA,sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu na udugu, uhuru, kujitegemea, haki, usawa, amani na utulivu, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu" Ni wenye mapenzi mema tu na nchi yao ndiyo wanajali kupiga hatua mbele na siyo kurudi nyuma kama wewe unavyotaka kuwa kikwazo cha nchi yako kupiga hatua. Nawasihi Watanzania wasibezwe kwa namna yeyote na watu ambao naamini hawana nia ya dhati kujenga Tanzania kwa maslahi wengi.
naiomba sana serikali ya chama changu. Iheshimu suala hili nyeti la katiba mpya. Katiba ni moyo wa nchi. Si jambo la kuletewa mzaha na maigizo. Nimesikitishwa sana na nilichoshuhudia kuhusu nakala za katiba inayopendekezwa. Kimeniuma sana. Nimelia kuililia nchi yangu inayoelekea shimoni.
Nimeshuhudia nakala za katiba zikiwafikia wananchi. Nimeshuhudia wananchi wakisoma kwa zamu,kwa saa chache,halafu nakala hiyohiyo kuhamishwa kwenda nyumba nyingine. Nimeshuhudia katiba inayopendekezwa ikisomwa kama gazeti. Nikalia sana.
Nimesikitishwa na mtazamo wa serikali kuwa wananchi wanatakiwa kuiona na kuisoma tu katiba inayopendekezwa. Si kuielewa ili kuchagua upande sahihi kwenye kura ya maoni. Huu ni mtazamo hasi na wenye ukakasi. Ni mtazamo wa kiutani,kisanii na kimaigizo. Katiba ni nyaraka ya kisheria. Hata wasomi wenyewe waweza kuisoma na wasielewe. Seuse wananchi wa kawaida?
Serikali,tafadhalini,muwe makini. Kucheza na katiba ni kuchezea moyo wa tanzania. Tujirekebishe na tustopishe hima!
Mzee tupatupa wa lumumba,dar es salaam
naona account yako umeianzisha maalum kwaajili ya kutetea upumbavu unaofanywa na serikali. Sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu asiyeelewa wingi wa watanzania wasiokuwa na uwezo wa kuielewa katiba kulinganisha na wenye uwezo huo. Kama kinana aliwauliza maji na katiba wanataka nini wakasema maji, sasa kuna uelewa hapo?