Je anakibali cha kuishi na kufanya kazi nchini?
Huyo ni Mganda ambae amesomea Sheria UDSM na amelowea hapa Tanzania sababu kubebwa na wanawake,kazi yake kubwa ni utangazaji alianzia EATV na sasa amekimbilia Magic FM.Lazima ajikombe kwa Magamba sababu anajua akienda kinyume tu,kesho hatakuwepo hapo alipo,ila akae akijua nguvu ya umma haitamuacha acha aropoke tu..atajuta na maneno yake atayatapika hapo
Jamaa nasikia ni raia wa Uganda. Mashambulizi yake kwa m4c yameegemea wapi?
Nafuatilia kipindi cha makutano show magic fm muda huu saa 9 na robo alasili hii,, kuna huyu jamaa anaitwa sebo anashambulia CDM kama mtu aliyetumwa, anazungumzia vurugu na mauaji ya morogogoro ya ally zona , kwa maongezi yake ni kuwa cdm wamevunja sheria na anaelemea upande wa kamanda shilogile, pia anasema M4C Chadema wamekopi na kupaste kutoka A4C ya kiiza besigye wa uganda.namsikiliza hapa 93.3 dom.katumia maneno makali mpaka fina mango akamwambia yeye hayupo yakimgeukia hayo maneno: kwa anayejua lolote kuhusu huyu SEBO please nahisi pengine ni product ya lumumba!
Huyu Mganda Sebo iweje achangie mijadara ki-negative ya siasa nchi? Je uganda kwao huko anaisaidiaje kisiasa? Hv huyu mtu kwanin amefanya kazi tz kwa mda mrefu hivyo? Hakuna mtz wa kum-replace? Jamaa ni jitu la majungu sana hili na sherehe nyingi sana za wizara na magamba huwa wanamualika.