Wewe unaikuza sana hii agenda kuliko uhalisia, mie mdogo wangu yuko pale mwaaka wa kwanza hilo ongezeko ni la kawaida sana tatizo labda hawakujulishwa mapema. Uelewe maisha yanapanda na gharama zake ndiyo maana watu wanadai kuongezewa mishahara kila wakati.
Unazungumzia hostel za nje za akina nani? tafadhali usipige siasa, laki tatu ya hostel za SAUT zina uhakika zaidi wa usalama, usafi na hata umeme, hizo za nje za gharama nafuu sijui ziko sehemu gani maana hata SWEA ma Luchelele huwezi pata gharama ya chini ya laki tatu labda siyo hostel ni nyumba mbovu mbovu za mitaani. Kwa mtu makini, atapenda mwanae ama mdogo wake akae za ndani. Mie mbeba mabox sioni tatizo kumtumia mdogo wangu Euros 150 kama ada ya pango naelewa matatizo ya kukaa nje ya chuo.