Na wanakuwaga na mbwembwe na kutaja mishara mikubwa ila sasa unatakiwa uwe na moyo na ujue kuongea na kushawishi
hahaha dada
feitty, hiyo kazi ni noma sana. Inabidi ujitoe ufahamu kabisa, ubraza-kaka or udada-duu tupa kule. Na inabidi mtu asiwe ana afya mgogoro, maana jua lote linamkaanga!
Halafu walivyo wapuuzi sasa, eti moja ya qualification ni ''Must be
fluent in English & Swahili''
π. Mtu anaenda kutembeza majagi na mapeseni huko Tandale kwa Tumbo, english my foot!!
Na wanataka mtu
SMART eti, tai na sharti safi nyeupe or blue. Mtu anakula vumbi chochoro zote mtaa kwa mtaa, plus jua kali, plus anashindia maji ya kandoro with kashata, uSMART/USAFI utoke wapi hapo?!!
Waduwanzi sana hawa wenye vikampuni uchwara vya kinyonyaji. Unalipwa per day kwa asilimia kutoka kwenye mauzo yako ya siku. So, uwezo wako wa kushawishi wateja ndo riziki yako. Hapo inabidi uwe na strong Art of 'kabobo' ili kushawishi watu wanunue. Otherwise utapauka na jua la kutwa nzima na end of ze day unarudi geto with buku mbili mfukoni.
π
Nina friends zangu wawili, wana wa kitaa, waliwahi kujaribu hiki 'kibarua'. Siku MOJA tu wakanyoosha mikono juu. Kesho yake mida ya jioni tupo maskani na wana, mmoja akawa anatusimulia experience aliyoiona huko 'kibaruani, akasema "Daaah ebana wana eeeh, ile kazi ya kishenzi hatari. Kutwa nzima sikuuza ata kijiko, nikashinda njaa. Nikanywa kandoro moja. Nusura nizimie. Tai niliiona nzito shingoni ''.
πππ
-Kaveli-