Ewe mungu baba mwenyezi mwingi wa Rehema, uliyeumba dunia watu na vyote vilivyomo.
Ukawapa wanadamu uwezo wa kufikiri na kutenda, na katikati yao ukaweka viongozi ili waweze kuwaongoza vyema watu wako.
Tunakushukuru eeeh mungu mwenye enzi kwa kutulinda na kututunza kwa mwaka 2018 dhidi ya maadui wetu wa mtandao pendwa uliobaki pekee ukikemea maovu yote chini ya jua na viongozi wake.
Kwa maana ni kwa NEEMA yako tunaendelea kutumia njia hii ya kupashana habari kwa maana njia zingine ama watu waliojaribu kuusema na kusimamia kweli yako binadamu waliojipa mamlaka ya kimbingu waliwafanya mateka, kuwatesa na hata kuua, na kwa maana hiyo basi tunamuombea kiongozi wa mtandao huu ( Maxence Melo), tunawaombea pia wahanga wa kusema kweli yako. Tundu Lissu, Ben Saanane, Azory Gwanda nk. Pia kawape MOYO mkuu waliowekwa mahabusu ama kufungwa kwa sababu za kisiasa.
Eeehe mwenyezi mungu baba wa amani, tunakuomba kwa utukufu wako kalinde nakuusimamia mtandao huu kwa mwaka 2019 na wanachama wake, na zaidi katupe HEKIMA ya kuendelea kusema kweli bila kuogopa binadamu awaye yote, zaidi tunakuomba eeh baba wape viongozi wetu HEKIMA na maarifa ya kutuongoza vyema ili tuendekee kuwa na amani, mshikamano na utengano kwenye taifa letu.
Amina!
Sent using
Jamii Forums mobile app