Ukata wa vilabu nao unafikiriwa, kuitunza timu kwa miezi tisa mfululizo huku ikiwa inacheza mechi ni jambo gumu. Pia wanachukua advantage ya mazingira, kwamba ukienda Kanda ya Ziwa umalizane na timu zote za huko, au wa mikoani wakija Dar wanamalizana na timu zote za huku, ndio maana vioja vya timu fulani kuanza ugenini mechi zao zote havyeshi...
Haya yatakuwa sawa endapo timu zote zitakuwa na uwezo wa kuhudumia timu kwa kipindi chote cha mwaka na kusafiri kwa kutumia ndege, usafiri ambao hauchoshi.