Nampongeza aliyebuni jukwaa la chit-chat.Hakuna stress wala kununiana.
Unaingia unatoa viblahblah vyako vya dizaini yoyote kisha unasign off.
Umemaliza, na hakuna mod atakayekukunjia ndita eti sijui umrvunja
sheria ya jf.
Kama hii thread ninayoandika. blahblah moja kavu sana ila yenye sababu
kubwa mno Invisible ndiye pekee anayeijua sababu ya thread hii.
Kama huna ishu kwenye siasa au jamii photos njoo chit-chat utuambie
kwa nini ukipiga miayo unatoa sauti.
Ngoja nikusaidie kukupa kidokezo cha thread nzuri ya chit-chat.
Lete thread ya kueleza/kushangaa kwa nini:
1.Umeme hauna kiuno lakini unakatika sana.
2.Msichana akivunja ungo hagombezwi kwa kuharibu chombo muhimu na mama yake
huendelea kupepeta mchele kwa kutumia ungo.