Haya mambo yalikuwepo toka enzi za utoto wangu, time table ya public transport pia zilikuwepo vituoni kama ulaya, enzi hizo public transport tuliita hekarus (mliokula chumvi kama mimi mtakumbuka haya).
Nakumbuka tulikuwa na school buses. Nilihudhuria ufunguzi wa yale mabasi, tena mabasi mapya yalituchukua toka mashuleni mpaka Karimjee. Tukacheza sana disco uwanjani tukiwa na uniform zetu, soda pia tulikunywa sana siku hiyo.
Masikini kumbe ile ndo ilikuwa mwisho wa kuyaona yale mabasi. Yote yalipotea, na huenda ndiyo zile DCM za mwazo kuwa private buses. Mungu utusaidie.
Hivyo kurudia tena sanduku za posta majumbuni ni jambo jema, lakini siyo ngeni sana, swala je maeneo ya ugavi wa barua yanafikika??? Utaipata barua yako kweli??
Kwa kweli Tanzania tumechanganyikiwa hatujui pa kushika sasa, tunatapatap kama mfa maji, nchi giza, baranara ndo hivyo tena, uchafu ni nyumbani kwetu. Mi nadhani tungesafisha kwanza nchi ndipo ufuate ugavi barua majumbani, maana mgawaji atapita uchochoroni na kwenye madimbwi chungu nzima??.
Kila la heri ktk juhudi za kulibomoa Taifa.