Pesa inani-control mimi

Cruel mpole

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
282
Reaction score
106
Nimekuwa nikijaribu kuzicontrol pesa,lakini zoezi hili limenishinda mpaka najikuta pesa ndio inaniendesha mimi badala ya mimi kuicontrol nakujikuta nafanya mipango ambayo sikutarajia mara niipatapo.

Pindi inapokwisha ndio mipango na mawazo mazuri yakimaisha ndio yanajaa kwenye fikra,chakushangaza ninapoikamatia pesa,malengo na mipango yangu ya maana niliyoipanga awali inapotea na kujikuta nafanya vitu tofauti ambavyo havina maana kama kunywa na kununulia watu pombe,luxury needs za hapa na pale,

Na mara pesa inapokatika,utakuta hata dawa ya meno ndani sijanunu,ndipo nafsi yangu inapo anza kusononeka na kukumbuka jinsi nilivyokuwa nanunulia watu pombe,na mbaya zaidi ninapokwenda kulia shida kwa watu hawa,hakuna hata mmoja anayeweza kunisaidia,nikaona si bure,niachane na pombe,lakini waapi,pesa inapokuja kwenye imaya yangu,nasahau yaliyonikuta nyuma nakwenda kujenga heshima bar.Nimekwishaona ni tatizo kubwa kwangu,lakini nimeshindwa kabisa.

Naomba ushauri wenu,kama kunanjia yoyoite ile itakayoweza kunisaidia ili niweze kuzicontrol pesa nakufanya mambo yangu ya maana,bila kuchelea.
 
cash ni liquid asset hakikisha huwi na cash ukizipata kimbiza bank
then ukiwa umekaa andika vitu muhimu unavyotaka ununue
hakikisha unapoenda kutoa uwe unatoa kiwango kinachotosha katika mahitaji ulioyanote tu USIZIDISHE
na unapoenda bar panga utakunywa bia ngapi na nyama choma kiasi gani piga mahesabu yako jumla itakuwa ni sh ngapi na beba hela hiyo tu itakayokutosha hii itakuepusha kutoa ovyo offer
 
Anza tabia ya kunywa nyumbani kila kitu nikuamua tu kama kweli umechukia hiyo tabia utaacha pia epuka kampani za walevi
 
Aisee km nakufahamu vile natamani nijue uko wp.

Poa hapo jambo la msingi ni kumshirikisha mtu wa karibu tatizo lako mfano ndugu unaemuamini, mke/mpenzi wako. Mshirikishe malengo yako, mueleze mpango wako wa kupata pesa na unatamani ukipata utimize kitu gani kati ya malengo uliojiwekea, muombe akusaidie mara tu utakapopata pesa akusaidie kukamilisha lengo hilo.

LAKINI hili litawezekana iwapo ukipata pesa huwi na kiburi. Maana kuna wengine utakuta mmekubaliana vizuri mkumbushe sasa uone matusi yake na kukwambia "pesa tulisaidiana kutafuta". Change ni wewe
 
pole sana, chukia hali hiyo toka moyoni mwako halafu amua kubadilika kabisa, usipende kuwa na cash, badilisha marafiki tafuta marafiki wenye mtazamo mzur wa maendeleo tena ikibidi wasiokunywa au wanaokunywa mara chache, andika vitu unavyotaka kufanya hakikisha km unaenda kutoa hela toa hela ya kitu unachohitaj tu, pili amua kuwa mtu wa ibada mshirikishe Mungu kwa kila jambo. Je umeoa/olewa??
 
umesema nilichokua nataka kumshauri... kila kitu ni kuweka nia. ukishajiona huwezi kukaa na cash mfukoni... usizitoe bank...

Niliwahi kuwa na shida kama hii siku za nyuma ... nikawa nataka kununua kitu kilichohitaji hela nyingi ikanipasa nilimbikize hela... kwa kuwa niliona sikuwa mwangalifu kipindi iko.. nilifungua account benki ambayo naruhusiwa kutoa mara moja kila baada ya miezi mitatu... mwezi wa kwanza baada ya kufungua nikawa nimeipungukia na cash siku flani hivi .. kila saa mawazo yakawa yananijia ''umeweka hela kule afu unasumbuka sasa, kachukue tu hapo then huchukui tena... kila mara yananijia haya mawazo''

Nilichofanya nikaenda kutoa 50,000 ili katika miezi mitatu inayofuata sitaruhusiwa kutoa, nikawa naweka hela miezi mitatu ilivyoisha nikaenda tena kutoa 50,000 ili inizuie kutoa the next 3 months... baada ya hapo nikawa nimeshazoa na kupata adabu ya savings.


 
jaribu kutoa fungu la kumi kwa Muumba wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…