Pesa au penzi

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Posts
8,597
Reaction score
1,693
Huwezi kuongelewa mapenzi bila kutaja suala la pesa. Wapo watu ambao wanaamini kuwa na pesa nyingi, nyingi kabisa za kutosha husaidia penzi kuwa imara na linaloridhisha.
Hata hivyo tumeona penzi la uhakika hata wakati pesa zikiwa hazipo au tumeona penzi la kweli hata katikati ya umaskini uliokithiri.
Hii haina maana kwamba pesa siyo muhimu, pesa ni muhimu sana. Na pesa ina umuhimu kwa kila mahusiano hata, hivyo inabidi ujiulize mwenyewe je, upo kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Utakuwa mtu wa maana sana kama utakuwa unatazama na kuwekeza kwenye penzi la kweli na si pesa.
Pia ni vizuri kuwa makini na mtazamo wa mpenzi wako je yupo kwako kwa ajili ya pesa au kwa ajili ya penzi la kweli.
Mtazamo wake kuhusu pesa ni muhimu sana.



AMEN..............!
 
Penzi ni engine, pesa ni matairi!
 
Jamani bila kificho mapenzi bila pesa hata kidogo haiwi...
 
kamwe hutaolewa utaendelea kutumiwa na kila mtu
Unanchekesha! nna mumewangu na wanangu,lakini ukweli unabaki pale pale kubali ukatae,ivi mwanamme akose hata hela ya daladala bado unakaa kisa unapenda? ubu fikiri tena....
 
Unanchekesha! nna mumewangu na wanangu,lakini ukweli unabaki pale pale kubali ukatae,ivi mwanamme akose hata hela ya daladala bado unakaa kisa unapenda? ubu fikiri tena....

Some people take JF very seriously!
 
Pesa ina umuhimu hasa pale wawil wanapokuwa na future, nani atapenda azae na kulea watoto katika umaskin? So pesa ni muhimu katika kujenga future yenu,ictoshe umaskin ni laana hakuna furaha ktk umaskini ni kujidanganya tu
 
Penzi muhimu, until you are played. Halafu ndo utaona kungekuwa na pesa basi unapata comfort (ufanye hata shopping kuondoa mastress). Hata sasa hivi usidanganyike people do not marry for love alone, though its a good thing to have.
 
Ukiyachonga, ukiwa speed yatapasuka, au utaita ajali kazini?:A S confused:

Hapo sasa, tafakari chukua hatua................!
Kwa hisani ya kimbweka.............!:A S 39:
 
Nimefunga ndoa na pesa, mwanamke akijilengesha, naingia kwenye mahusiano naye lkn mawazo yote na upendo wote unabaki kwa mke wangu PESA.
 
Pesa ni muhimu na pia inamaintain uaminifu ndani ya penzi.
 
Asilimia kubwa wanawake ndo wanapenda dezo, kwa hiyo penzi na pesa inaegemea kwa jinsia ya kike. Mwanaume humpenda mwanamke bila kuangalia ana pesa au la..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…