Permaculture - muhimu kwa mazingira

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
PERMACULTURE

Nimegundua vitabu vingi vya Permaculture duniani kote, vimeandikwa kwa kiingereza, kijerumani, na lugha nyingine ambako zaidi ndiko kazi za Permaculture zilikoanzia na zinakoendelea kuendelezwa.

Kwa kuzingatia kwamba wakulima wengi walioanza kujifunza kilimo kwa kufuata mfumo au maelekezo ya Permaculture walioko katika nchi za Afrika mashariki wengi wao wamefundishwa kwa Kiswahili, lakini pia Kiswahili ni lugha inayoeleweka kwa urahisi zaidi kwao, kwa kuwa napenda elimu na ujuzi uwafikie watu wengi na kwa muda mfupi nimeona umuhimu mkubwa wa kukiandika kwa Kiswahili andiko la Permaculture ili liweze kutatua baadhi ya changamoto kwa wakulima wetu.

Kutokana na kupatikana kwa andiko hili la Kiswahili matarajio yetu ni kwamba kutakuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye mambo ya afya, na uhifadhi wa mazingira. Maana watu wengi wamepotea kwa kukosa maarifa. Elimu na mafundisho yaliyomo katika kitabu hiki itawafikia watu wengi zaidi na ikifanyiwa utekelezaji Wengi wataepuka kilimo chenye kutumia kemikali kwa wingi kitu ambacho kimepelekea kuwa chanzo kikubwa cha matatizo ya kiafya lakini pia uchafuzi wa mazingira.

Nimekiandika kwa namna ambayo wewe mwenyewe msomaji utapata mwongozo katika kufanya utekelezaji katika kuanza kukibadilisha kilimo chako, na mfumo mzima wa namna yako ya kuishi na hivyo itapelekea wewe na familia yako wote kuwa na afya bora na pia kuwa na mazingira mazuri na salama.

Andiko hili litakuwa likiendelea kufundishwa hapa JF kila siku ya Alhamisi. Fuatana nami ili uweze kujifunza mengi kuhusu permaculture.

Permaculture nini?

Ni njia mbali mbali za kuweka mfumo endelevu wa maisha. Ni wajibu wako kujenga mfumo wa kujitegemea mwenyewe katika kujiletea maendeleo, kuyatunza mazingira na kulinda pia viumbe wengine.

Permaculture ni mjumusho wa jinsi aina mbalimbali ya viumbe wanavyoweza kuishi pasipo kuleta uharibifu na kukuza uchumi. Hii ni njia sahihi ya kuishi maisha kwa uhalisia wake.


Ni nini kinawafanya watu wengi (hasa watanzania) kuendelea kuwa wategemezi?

Hizi ndizo sababu kuu zinazowafanya watu wengi kuendelea kuwa wategemezi:-
  • Ukosefu wa elimu
  • Utegemezi wa kutumia mbegu chotara na mbolea za viwandani zenye kemikali
  • Kutegemea maelekezo kutoka kwenye makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako
  • Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara na mabenki
Nini kifanyike: Kila mtu anao wajibu wa kusimamia kuwa na afya bora na kulima / kusitawisha mazao yako mwenyewe. Wajibu huu ni sawa na kuchapisha fedha zako mwenyewe. Hakuna kitu kinarudisha maendeleo ya watu nyuma kama afya mgogoro.

…. Tunaendelea tena wiki ijayo … Ahsante kwa kusoma hadi hapo. Kama kuna maswali yawekwe hapa ili tupate majibu yake kabla ya kipindi kinachofuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…