Over 250,000 youths petition Parliament over constitutional amendment

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,468
Reaction score
38,203
Heshima sana wanajamvi,

Kumekuwa na laana ya kiu ya watawala wengi wa Afrika kutaka kutawala hata kama katiba za nchi zao zimeweka bayana uko wa uongozi.Rais Paul Kagame ambae aliivamia Rwanda akitokea Uganda mwaka 1994 na kushika madaraka ya makamu wa Rais na waziri wa ulinzi kuanzia mwaka 1994 - 2000.Kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2015 amekuwa rais wa taifa hilo dogo sana na lenye msongamano wa watu barani Afrika.Ikumbukwe hata mwaka 1994 hadi mwaka 2000 alipokuwa akishika wadhifa wa makamu wa Rais na waziri wa ulindi yeye ndie alikuwa kiongozi mkuu huku Rais Bizimungu akiwa hana mamlaka wala maamuzi yoyote.

Pamoja na Rais Gen Kagame kutawala Rwanda kwa zaidi ya miaka 26 lakini bado hajaridhika kuachia madaraka.Vijana wa RPF sasa wapo mbioni kuhakikisha kila mbinu chafu inatumiwa katiba ya Rwanda inavunjwe ili Kagame aongezewe muda wa kutawala Rwanda unaomalizika 2017.

Marais wa nchi kadhaa tayari wameshaanza mchakato wa kubadili katiba ili waendelee kubakia madarakani milele hadi Mwenyezi Mungu atakapowachukua.Rais Museveni wa Uganda,Rais Nkurunzinza wa Burundi tayari wameshachukua hatua ya kujibakisha madaraka kwa kubadili katiba za nchi zao.
 

Attachments

  • 1432245163The-youths-upon-arrival-at-Parliament-Buildings-where-they-delivered-boxes-full-of-ind.jpg
    61.4 KB · Views: 54
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…