Onyo from the British!

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Membe angekua na akili hata za kuazima toka kwa Mkullo wizara ya mambo ya ndani wangekuwa na website ya kutuonya kuhusu UK na haswa kutuambia:

WAINGEREZA WANAONGOZA KWA KULAWITI WATOTO WADOGO

WAINGEREZA WANAONGOZA KWA ULEVI MBWA

TUSITEMBELEE MAENEO KAMA READING AMBAKO NI RAHISI KUIBIWA BANK DETAILS ZETU

TUSITEMBELEE MAENEO YA PECKHAM NA SOUTH LONDON BILA KUSAHA HAU tot-nam AU WENYEWE WANAPAITA TOTTENHAM AU SEVEN SISTERS KWANI YANAONGOZA KWA VIJANA KUPIGA WATU VISU

BILA KUSAHAU KUWA SWINE FLU NDIO NYUMBANI KWAKE

etc etc



http://www.fco.gov.uk/en/travelling...advice-by-country/sub-saharan-africa/tanzania
 


GT

Kwa nini ni rahisi kuibiwa Bank Details ukitembelea Reading?
 
Matatizo yaliyokuwepo TZ hatujayamaliza, unataka tuanze beef na UK?
 
Is this any better?

wamarekani
 
TUSITEMBELEE MAENEO KAMA READING AMBAKO NI RAHISI KUIBIWA BANK DETAILS ZETU
bank details unaibiwa na wazungu, wanigeria, watanzania, wapolish au wajamaica?? nani kati ya hawa ndiyo anaiba bank details, weka bayana
 
Kama ni issue ya crimes mi nadhani GT uwe muwazi tu kwamba nchi yoyote duniani lazima iwatahadharishe wananchi wake juu ya usalama wao wanapotembelea nchi nyingine.

Mimi bahati nzuri nilipokwenda India kwa mara ya kwanza Ubalozi wetu pale New Delhi walinipa kijitabu kinacho eleza ni maeneo gani hayafai kwa wageni ndani ya India.

Sasa issue ipo kwa uzembe wa wizara ya mambo ya nje ya Tanzania (Membe) na wachini yake kwa sababu ni wajibu wa wizara kuweka wazi taarifa kwenye website ya wizara security issues and threats kwa waTZ wanapotembelea nchi za ng'ambo.

Wala UK au USA hawata lalamika ukiweka taarifa hizo kwani wao wanafanya hivyo kuwalinda raia wao na wewe (membe) utakuwa unafanya hivyo kulinda raia wako.

GT, Tanzania (membe) hajazuiwa kuweka taarifa za usalama kwa watanzania wanapotembelea UK au USA au hata Kenya lakini uzembe au kufikiri kuwa ulaya hakuna uhalifu ndo kina mfanya membe aone kuwa hakuna tatizo.

Lakini mwisho, ni kweli kwamba tuna security problems/weaknesses zaidi kuliko nchi zilizo endelea na kazi kubwa inahitajika.
 
Membe angekua na akili hata za kuazima toka kwa Mkullo wizara ya mambo ya ndani wangekuwa na website ya kutuonya kuhusu UK na haswa kutuambia:

WAINGEREZA WANAONGOZA KWA KULAWITI WATOTO WADOGO

Hii si inatokea hata Tanzania? Na hata nchi zingine duniani?

WAINGEREZA WANAONGOZA KWA ULEVI MBWA

Ulevi una watu wake. Sasa kwa Ulaya bei za pombe ni rahisi sana na vijana wa UK hupenda kunywa kupita kiasi hasa wakati wa weekend, kwa sababu wakati woote wa wiki nzima huwa wanachapa kazi kulea uchumi wa nchi yao ambao mpaka sasa unayumba kidogo na idadi ya unemployment imeongozeka kwa asilimia kubwa.

TUSITEMBELEE MAENEO KAMA READING AMBAKO NI RAHISI KUIBIWA BANK DETAILS ZETU.

Huu mkuu ni uongo mkubwa sana. Mimi nimewahi kuishi katika kamji haka ka Reading na kuna watanzania wengi tu wanaishi. Hakuna mambo uloeleza. Tena kamji haka kanaweza kulingana hata na mji wa Dar-es-salaam. Wakazi wake ni watu mchangayiko na kuna shopping centre kubwa maarufu kwa jina la The Oracle. Pia kamji haka kana ofisi kubwa ya watengeneza software ya Oracle inayohusiana na masuala ya "database".

TUSITEMBELEE MAENEO YA PECKHAM NA SOUTH LONDON BILA KUSAHA HAU tot-nam AU WENYEWE WANAPAITA TOTTENHAM AU SEVEN SISTERS KWANI YANAONGOZA KWA VIJANA KUPIGA WATU VISU.

Hii pia si kweli kwani watu wengi tu wanatembelea maeneo haya na pia haya maeneo yote uloyataja pia nimeishi tena kwa muda mrefu na pia kuna watanzania wengi sana. Cha msingi tu ni kwamba haya maeneo ni yana wahuni sawa tu na Manzese ambao wengi ni wa asili ya Afrika na Carribean. Ila pia maeneo yoote haya yana watu wenye asili ya Afrika kwa wingi na vyakula vya kutoka Afrika ni vingi mno kuanzia unga wa sembe, ulezi,maembe, mapapai na kadhalika

BILA KUSAHAU KUWA SWINE FLU NDIO NYUMBANI KWAKE

Hii ya mafua ya Swine ni kwamba umeanzia South East Asia na kuelekea hadi Mexico kabla ya kutua UK. Wale wasafiri hasa wale "holiday makers"ndio wamekuwa waenezaji wa ugonjwa huu hasa wale wanaotokea hayo maeneo niliyoyataja.

Kwa kweli mkuu GT haya ulioyaleta hapa naweza kusema ni "very serious allegations" na inabidi utafakari kidogo.

Halafu ni nani ametoa maonyo haya? na je una source yoyote?
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…