Wakuu,
katika udadisi wangu mdogo nimegundua kuwa pamoja na watumishi wengi wa Serikali kutotaka kuhamia Dodoma, lakini wapo Viongozi wao wanaofikia hatua za kutunga/kuunda vikwazo na kujenga hoja kuwa kutokana na u-special wao, waendelee kukakaa Dar.
Naamini tunajua baadhi ya taasisi hizi na sababu zao za kuji-pretend kuwa special. Kwa taarifa zangu, sababu zinazotumiwa sana ni pamoja na kuwa:
1. Hawawezi kuhamisha miundombinu haraka au Dodoma haina uwezo kuweka miundombinu yao ,
2. Fedha za kuweka miundombinu hiyo e.g. stores, maabara, safes & security sysstems, etc. hazipo
3. Wanategemeana mashirika ya kimataifa kuendesha shughuli zaonyingi hivyo hawawezi kuhamia Dodoma wakati mashirika hayo bado yapo DAR.
Na sababu nyinginezo;
Cha ajabu ni kwamba taasisi nyingine zenye nature hiyohiyo tayari zipo Dodoma, au viongozi tayari wapo Dodoma na Dar wamebaki watendaji/wataalamu tu.
Hebu tutaje taasisi hizo hapa na ikiwezekana Wakurugenzi wake wanaotumia ujanja kubaki Dar, ili Serikali ijue "KIKULACHO" kilicho nguoni.
Karibuni.