wanajamvi kwa maoni yangu naona ni wakati mwafaka sasa wa kutenganisha siasa na jeshi.liwe la polisi,jwtz,magereza...
kwasababu mlinda usalama huyu anapogombea au anapoteuliwa na chama tawala katika nafasi yoyote sarikalini,inaonekana ni sawa na nihaki.
Lakini mlinda usalama huyu anapoamua kujiunga na vyama vya upinzani anaonekana ni mhaini na msaliti katika nchi yake au anaendesha mapinduzi.
rejea katika utawala wa Mkapa ( IMRANI KOMBE ) alipouwawa kwa kisingizio kuwa alifananishwa na jambazi sugu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu.
Ni wakati sasa kwa katiba mpya ichague moja.kuwaondoa kabisa katika ulingo wa siasa au itamke wazi kuwa ni ruksa kwao kujiunga na kugombea nafasi mbalimbali katika vyama vya upinzani nchini.