Kikarara78
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 1,495
- 901
Du simple tu wanayotumia matumbo ni wale waliyotufikisha hapa tulipo kwenye mikataba mibovu ya ten % richmond then dowans then symbion wapo viongozi ccm wazuri sana ila chama kina misingi yange ukiwa nje utaona uozo mwingi sana ukishaingia kila utakachotaka kiwekwe sawa ni cha mkubwa fulani na ukitaka kukiona cha moto ifwatilie vizuri utapata hata ajali ya kugongwa na bajaji
Sijakataa hilo wala kubisha, hoja yangu ni kuwa ni sawa kusema ni wao tu ndio wanaotumia AKILI ??? Alikuwa au walikuwa wapi miaka, muda wote huo mpaka waone mambo yanakwenda kombo, hovyo ndio waje na Kauli hii ???
Yeye mwenyewe huyo Sitta anafikiri kwa kutumia tumbo. Wanaofikiri kwa kutumia akili wapo Cdm kasoro Shibuda.Habari zenu Great Thinker,Naomba kujua hasa nini maana ya hii kauli ya Mheshimiwa Sitta aliyoitoa Mbeya kuwa wao waliokuwa kwenye Mkutano, Kongamano wanatumia Akili na siyo tumbo ?? Ana maana kwenye Chama chao cha CCM na Serikali wengine wote wanatumia tumbo kufikiri na kutoa maamuzi ?? Hata Kiongozi wetu wa Nchi nae anatumia tumbo ???? Maana Rais wetu akuwepo Mbeya."Nawapa matumaini katika chama chetu kuwa sisi mnaotuona hapa ndio tunaotumia akili siyo tumbo katika kufikiri, hivyo chama chetu kitakwenda vizuri,"aliongeza Sitta.Tuzidi kuombea Nchi yetu maana Viongozi wetu na kauli zao zinatutatiza sisi WananchiNawakilishaSource: Mwananchi - Sitta amkaba koo Ngeleja , ATAKA WALIOSABISHA MGAWO WAWAJIBISHWE
Yeye Sitta na Mwakyembe ndiyo wanastahili kuwajibishwa, Sitta alilizima sakata la Richmond kihuni habla Serikali haijatekeleza maazimio ya bunge kuwawajibisha wote waliohusika, na Mwakyembe kwa kinywa chake alikiri kuwa kamati yake ilificha taarifa muhimu kwa kile alichoita kulinda heshima ya serikali.Hawa ni wanafiki wakubwa walifanya waliyofanya kwa kushirikisha matumbo yao badala ya akili zao, magamba ni magamba tu kamwe hayawezi kuwa ngozi.
Daima binadamu(mwanaume) hasahasa tunavchwa viwili cha juu na chini sasa hawa wenzetu magamba wanafikiria kwa kichwa cha chini.