Nimerudi tena msakatonge mimi

monotheist

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
887
Reaction score
1,596
Habari wakuu

Mimi ni mhanga wa ajira/kibarua nimetafuta kazi katika makampuni tofauti lakini sijafanikiwa baazi ya makampuni yalihitaji nitoe pesa ili nipate kazi kwa kweli hili swala kwa upande wangu ni gumu na huu ni mwaka wa pili sasa nimekua kiguu na njia bila mafanikio

Elimu yangu ni kidato cha sita nimeshindwa kuendelea na elimu ya juu sababu ya ukata wa pesa na sina tena matumaini ya kuendelea

Nilishawahi kufanya kazi ya usafi katika makampuni mbalimbali hapa Dar na pia nilishawahi kufanya kazi za hoteli katika vitengo tofauti

Maisha yamekua magumu mno sina chochote cha maana nnachomiliki zaidi ya simu yangu ya tochi na mavazi mpaka sasa nina umri wa miaka 26

Nahitaji msaada wenu tafadhali nipo tayari kufanya kazi yoyote kwa kampuni au mtu yeyote ili hali iwe kazi ya halali

kwa yeyote atakayeguswa ani-PM tafadhali

AHSANTENI.
 
Mkuu ajira ni bomu haswa kila sehemu ni kilio, kama huna Godfather ndo kabisa, halafu nimepitia file lako nimeona unauza mayai sijui kuku na baadhi ya vitu, we komaa tu na ujasiriamali ukuze mtaji utafika tu maana kazi utakazopata ni unskilled ambazo malipo ni hand to mouth with a lot of pressure.
 
,nafikiri sasa ni wakati wa hawa viongozi
kutuhimiza kuacha kupoteza muda na rasilimali
zetu mashuleni na vyuoni maana hivi vijihela
tunavyoharibu kama ada ni mtaji tosha kabisa.
 
ni kweli nilikua mfugaji ila mtaji umekata natafuta pesa ya kuanza upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…