Nimeikuta kwenye blog

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
25,556
Reaction score
25,371
WIZARA YA MICHEZO INASTAHILI
KUWAJIBIKA KWA NANI?; VYAMA VYA
MICHEZO AMA TAASISI ISIYO YA
KISERIKALI?
Hivi
karibuni
Chama
Cha
Tennis
Tanzania
(Tanzania Tennis Association) kilipitisha katiba yake na
kufanya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wake
baada ya miaka mingi ya udikteta ndani ya chama hicho.
Hata hivyo baada ya muda mfupi wa furaha kwa wapenzi
na wadau wa mchezo huo nchini, mzimu wa uongozi wa
zamani umeendelea kuikumba taasisi hiyo muhimu
katika michezo.
Katibu wa zamani (aliyelazimika kujiuzulu ) INGER NJAU
na mwenzake FABRIZIO CALDARONE wamekuja na
taasisi yao mpya ya ATP TENNIS FOR CHARITY ambapo
huko ulaya kuna taasisi inayofahamika kwa jina la
TENNIS FOR AFRICA , “ taasisi hizo mbili zenye majina
tofauti lakini zenye wanachama haohao ( Inger Njau na
Fabrizio Caldarone ) zina harufu ya utata” alisema
mjumbe moja ambaye hakupenda jina lake litajwe.
“Lakini utata zaidi ni pale ambapo mkurugenzi wa
michezo nchini LEONARD THADEO alipowapa kibali cha
kuendesha "shughuli za Tennis" kwa viongozi hao wa
kigeni na kutotoa fursa na ushirikiano stahiki kwa chama
chenye dhamana ya kusimamia mchezo wa Tennis
Tanzania” mtoa habari huyo aliendelea kuelezea.
UCHUNGUZI
ZAIDI: Hata hivyo
katika mkutano wa
kamati ya utendaji
wa chama hicho
uliofanyika hivi
karibuni mengi
yaliibuka kuhusu
uongozi uliopita,
ambao kimsingi
kiongozi huyo wa
zamani
aliyelazimika
kujiuzulu
akishirikiana na
raia mwingine wa
kigeni ndio hao
ambao taasisi yao
inayofanya kazi
sawa na majukumu
ya Tanzania Tennis
Association. Ilibainika kwamba siku tatu (3) tu kabla ya
uchaguzi mkuu kufanyika (19/6/2013) uongozi huo wa
zamani ulichota fedha benki (withdrawal) kiasi cha US
$: 12,000 sawa na TSH: 19,800,000/= pamoja na fedha
zingine za kitanzania ambazo idadi yake haikufahamika
mara moja, kimsingi waliamua kufanya hivyo kwa
sababu walijua kwamba uongozi wao unaelekea mwisho,
na kwamba uongozi mpya ukiingia hawataweza kutoa
fedha hizo benki kutokana na mabadiliko ya kiuongozi.
UONGOZI MPYA: Baada ya mjadala mkali kuhusu katiba
ya Chama Cha Tennis Tanzania kuvunjwa na fedha hizo
zilizotolewa na uongozi huo wa zamani, kumeonekana
kuwepo na mpasuko mkubwa kati ya wanaotaka kuacha
kuhoji fedha zilizotolewa kinyemela dhidi ya wale
wanaotaka kujua kulikoni?. “Lazima tujue sababu ya
fedha hizo kutolewa, nani anawalinda watu hao? , kwa
nini hadi sasa stakabadhi zote za kibenki (financial
documents) hazijakabidhiwa kwa uongozi mpya kama
alivyoahidi rais aliyepita kwenye mkutano mkuu wa
TTA uliopitisha katiba na kufanya uchaguzi?, kama
zimekabidhiwa; nani anawalinda wakwapua fedha za
chama wasiwajibishwe? iweje mpaka sasa uongozi
mpya hauna majibu?” alihoji mtoa habari huyo
aliyeongea kwa uchungu kwa kujali masilahi ya mchezo
wa tennis. "KWA KUWA INGER NJAU AMENUKULIWA
AKISEMA KUWA ALIPEWA RUHUSA NA LEONARD
THADEO" JE MKURUGENZI HUYU WA MICHEZO NCHINI
ALISTAHILI KUTOA KIBALI CHA N.G.O KUFANYA KAZI
AMBAZO NI MAJUKUMU YA CHAMA CHA TENNIS
TANZANIA?. “Je mkurugenzi huyo wa michezo
anafahamu Conflict of Interest kati ya taasisi hizo mbili
za kigeni na chama chenye dhamana ya mchezo husika?,
ama pengine mkurugenzi hajali vilio vya watanzania bali
anajali vilio vya wageni kwa sababu anazozijua yeye?. Au
pengine mkurugenzi huyo anayo masilahi binafsi na
taasisi hiyo inayofungamana na taasisi iliyopo Ulaya?.
UTAIFA KWANZA: Muda sasa umefika wa viongozi
wenye mtazamo wa kimasilahi kusemewa waziwazi
sababu kama ni swala la mkurugenzi wa michezo nchini
historia yake ni ‘ndefu na mbaya balaa’!. Mfano mzuri
ni pale mkurugenzi huyo alipokuwa na uhusiano wa
kimasilahi na TOC ambapo wakati wa London Olympics
bosi huyo wa wizara aliona London ni rahisi kufika
kuliko Kibaha ambapo wadau walilalamika aende
kuhakiki hali ya kambi ya Riadha na hakwenda, lakini
London alikwenda haraka kuliko Super Sonic . ‘Itakuwa
ajabu kama mkurugenzi mmoja ataendelea
kuendekeza dalili za kifisadi wakati waziri na naibu
wake wakitulia kila kukicha’ . WAZIRI SIKILIZA VILIO
VYA WADAU WA MICHEZO; MAANA WAO NI WATU NA
SIYO VYURA; BINADAMU MWENYE AKILI TIMAMU
HAWEZI KULIA WALA KULALAMIKA BURE. Upande wa
riadha wadau wamelalamikia ufisadi uliosababisha
makampuni mawili ya kimataifa ( PUMA na LINING )
kutuita matapeli, mkurugenzi anayetajwa anafahamu
mwanzo mwisho yaliyojiri kuhusu makampuni hayo
mawili, kama hahusiki basi anawalinda waliohusika,
AMBAPO KISHERIA KUHUSIKA AMA KULINDA
i LA JINAI.
 
mkuu Gang Chomba, mizizi ya ubabaishaji imekomaa sana nchini Tanzania, inatakiwa jitihada za ziada zifanyike.
Sipendi Watanzania tunavyojisinga sifa mbaya kwa makosa ya wachache. Kwanza hata hao wanaosemwa kuwa wakwapuaji wengine sio Watanzania. Waswahili husema ubaya hauna kwao, yeyote anaweza kuwa. Labda tuseme taratibu za kuwadhibiti wabaya zina kasoro zaidi hapa kwetu kuliko kwengine kwingi. Tuhangaike kutafuta dawa ya hilo, si kujichafua kwa uroho wa wachache miongoni mwetu. Au nawe mdau Gang Chomba unajikubalisha kuwa ni miongoni mwa wababaishaji kwa sababu tu ni Mtanzania?
 

Huyu Gidabuday ni mzalendo mkubwa sana wa michezo hapa Bongo.
Ana siri nzito za ulaghai unaofanywa kwenye mabaraza na vyama vya michezo Tz.
Kipindi wanateua timu ya Olimpiki kuiwakilisha Tz aliapa akasema kama watarudi na medali atachoma moto vyeti vyake vyote na kurudi umasaini kuchunga ng'ombe. Nilipenda mkwara wake aliopiga ambao kiukweli timu ya riadha haikurudi na hata kitu mkononi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…