Nimeikimbia Tanzania

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,764
Baada ya kwenda ubaharia kiasi cha miaka kumina tatu nikatamani kurudi kwetu ,ni kipindi kirefu nimeondoka na hamu ya kurudi na kuangaza nyumbani imenijia ,na kweli melini inakuwa huna wala hufuatilii mambo ya nyumbani ni kama umepoetea vile ila wanajua upo hai ,sasa niliporudi ni kipindi kile ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi wanakamatwa na kufanyiwa unyama ,katika kibaraza hivi wakati gumzo hilo limetannda akazuka mmoja akasema na wenye vipara pia vichwa vyao dili ,dah moyo ulipasuka pah ,ila nilijichekesha na kubabaisha kama sie kwani tulikuwepo kama watu wanne hivi tuna vipara ila changu ndio kama kinaanza ,nikaibishia kama si kweli ,wakadakia wengine na kusema ni kweli tena bora uvae kofia ya nguvu la kama utatembea kichwa wazi basi jamaa watatia bei.

Siku ya pili nilihama mji baada ya wiki hawakuniona tena ,niliporudi nikaulizwa mbona mara nikawambia ile si nchi ya kuishi kwani huwezi kutofautisha kati ya simba na binadamu ,mpaka ngozi unachunwa ndipo nikaamini kama Tanzania ni nchi ya ajabu japo haijatangazwa rasmi.
 
Ha ha haaaaaa acha uwoga ww rudi kwenuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…