Habari wana jamii!
Mimi ni mmoja wa wale waliokuwa wanahangaika kutafuta kazi kupitia tume ya ajira, bahati kufikia mwezi mei mwaka huu nilibahatika kuitwa kwenye ajira baada ya kufaulu usahili wao. Tangazo la kuitwa kazini lilitujulisha kuwa barua za ajira zimetumwa kwenye anuani zetu za posta.
Nilisuburi takribani siku saba bila kupokea barua, baadae niliamua kwenda kuifata dar kwa kuwa niliwahi julishwa unaweza pewa copy ya barua. Nilipoifata wakanambia hawawezi kunipa nisubirie iliyotumwa, na kama sijaipata nirudi dar baada ya wiki mbili, walidai hayo ni maagizo ya bosi na wao hawawezi kiuka. Sikufurahi, nikaenda kumuona mkuu wao, na baada ya kujieleza aliwapigia simu kuwaambia kuwa wanipe barua.
Hamad!! napewa barua P.O. Box yangu imekosea imewekwa ya mkoa mwingine kabisa ambayo siifahamu kabisa, na kwa maana hiyo ningeisubiria ile barua mpaka milele nisiipate.
Basi nikaripoti kazini nikaelezwa kuwa kama ningeenda baada ya hizo wiki mbili ningekuwa nimechelewa na hivyo wangetangaza upya mchakato wa zile nafasi:
MY Take: Wale mnaopata ajira, ukiona umekaa bila kupokea barua haraka wahi ofisi ya ajira mapema sana, na hata wakikunyima barua, basi waombe wakutajie walitumia box gani, maana yangu inaonekana walikopi barua ya mtuvinginevyo unaweza kukosa ajira kwa ajili ya jambo kama hili