Kwa Mimi Fimbo/Kiboko kinafaa kutokana na Mazingira husika
Kwa mtu mwenye level Nzuri ya maisha ambayo inampa mtoto fursa ya kusoma shule nzuri (wanakutana watoto wa daraja moja) na hata nyumbani kuna kila kitu kizuri kinachomu update mtoto, hapo control ya mtoto huwa ni raisi na hata uelewa wake unapo mkanya anakuelewa bila fimbo
Tatizo linakuja huku uswahili, Mara kibaokata/mara mtu kasutwa, mara kafumaniwa nk, mazingira hayo kulea mtoto nishida sanasana na ukichangia na shule anayoenda kusoma anakutana na watoto wenzie wa ushwahili,
Mtoto anaweza kuja na kituko ambacho hata hamuwezi kukiangalia, lakini ukimwambia hiyo si sawa anakwambia mbona fulani kafanya hivi na mamake kacheka tu, kama hukuweka kiboko hapo ndio imetoka hiyo
mabanda ya Video yapo kila kona na hawachagui cha kuweka, unakuta mtoto mdogo kabisa lakini yupo kwenye picha ya ngono inayooneshwa kwenye hicho kibanda, ukimkataza kwa maneno naye ana argue, mbona fulani anaaangaliaga, Hapo bila kiboko kesho yupo tena
Kwa tuliokulia Uswazi, Kiboko ni njia sahihi kabisa, huwezi kumshauri ama kumkanya mtoto wa uswahilini kwa maneno tu,
SIJUHI KAMA NIMEELEWEKA NINAPOSEMA USWAHILI