mkuu magonjwa hayakwepeki kikubwa ni chanjo na matibabu, pakuzingatia usafi ni kuzingatia ili kuondo magonjwa hayo.
Idadi ya ngombe kubwa au ndogo si uhakika wa maziwa mengi, kikubwa mbegu nzuri kuanzia majike mpaka madume/dume.
Matunzo mazuri kuanzia lishe,chanjo na matibabu.
idadi ya wahudumu ni wawili, wanatosha kabisa ila wawe nanauelewa wa mifugo la sivyo watakupasua kichwa na ng'ombe utawaona ka adhabu kwako.
banda liwe la kawaida ila liwe na ukubwa wa kuwatosha ng'ombe wako katika namna ya kula na kulala pasipo kusongamana, ila liwe limezibwa juu lote au nusu pindi jua litakapokuwa kali waende kivulin/upande uloezekwa hivyo hivyo nyakati za mvua, pia ukumbuke sehemu ya kukamulia, uwe na sehemu ya kuweka ndama la sivyo utalia kila uchwao maana ndama watakuhujumu katika maziwa.
vitendea kazi ni ka hivyo ulivyokuwa watumia kwa kwa hao ng'ombe wa nje yana kamba ni muhimu hata ka ng'ombe wanakaa free bandani, vyombo vya chakula kwa ng'ombe. vyombo vya usafi. n.k.
Kila la heri mkuu