Acheni siasa/porojo za vijiweni
kwenye mambo ya kitaalam
kama elimu, tuachieni
wataalam tujadili na
kurekebisha dosari
zilizosababisha kufeli kwa form
four 2013! Nashangaa
MALUMPENI wamekurupuka
from no where kila mtu na
hoja zake dhaifu za vijiweni
mmesomea wapi ualimu au
mnadhani walimu
wanachaguliwa kwa kufumba
macho na kunyosha mikono
juu!!
dancani huyu jamaa ameikopy iyo post huko anapojua yeye na kaipaste hapa bila kuangalia topic inasemaje..Sijakuelewa mkuu hizo stori za vijiweni au siasa ni zipi kwenye hii thread wakati sisi tunajadili NECTA ilivyokosoa habari za haya magazeti tajwa
Mimi sipendi na wala sitawalaumu waandishi wa HABARI hata siku moja na nitakuwa wa mwisho pekee yangu kufanya hivyo. HUYU MKURUGENZI WA GREEN ACRES alidanganywa na CLOUDS RADIO kuhidhalilisha NECTA eti kwasababu NECTA WAMEWALALAMIKIWA WAO KWA KUMPROMOTE YULE DOGO MWAKA JANA ALIEANDIKA BONGO FLAVA KAMA SHUJAA. Sasa mwaka huu vijana wamemchukulia yule kijana kama role model wao then kuchora kwingi. Sasa waandishi wameripoti vile vielelezo alivyovitoa yule mkurugenzi ambayo pia ni journalism. Clouds ni radio ya MABWEGEEEEEEE
Chama kinachomiliki gazeti la Tanzania daima ni bora wakaligeuza kuwa gazeti la udaku litawafaa sana
Mimi nikisema hao Clouds wanapromote ufreemason nchi nzima watu wananuna
Wanasheria wanaandaa mashtaka dhidi ya Bujugo ya kuchafua jina la NECTA.Huyu mkurugenzi hana nidhamu hata kama ingekuwa ni kweli necta walikosea ilibidi afuate chain nzuri yeye akiwa kama mdau wa elimu ili kujua tatizo kabla hajakimbilia kwenye vyombo vya habari kupotosha uma kuhusu necta.mimi nadhani serikali ifike sehemu ichunguze na itengeneze mfumu sawa kwenye elimu..Hawa watu wanaojiita WAKURUGENZI,NA MAMENEJA Kwenye shule wanatoka wapi?kwa maana nyingine hizi ni kampuni na kampuni zipo kibiashara zaidi.Hii inadhibitishwa na baadhi ya wakurugenzi hao kuchukua matokeo ya mitihani na kuyatangaza kwenye vyombo vya habari ili wapate wateja.hii ni hatari miaka ya nyuma walikuwa wanafanya mbinu za kuiba mitihani ili shule zao zionekane zipo juu lakina baada ya mama NDALICHAKO kujitahidi kupunguza wizi huo kwakiwango kikubwa sasa wanajaribu kutafuta kila aina ya mbinu chafu ili kumharibia mama huyu aondolewe ili waendelee na mbinu zao chafu.nNDALICHAKO SONGA MBELE USIBABAISHWE
Pamoja sana mpaka mwisho wa dahari mkuu
Hii radio ingekuwa amri yangu ingefutwa, sio sherehe na matukio tu kwaajili ya wanafunzi bali hata kuharibu lugha, kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vibaya na kuwapopurize kama yule wa mwaka jana, vijana kuacha shule na kuwainingiza kwenye the so-called THT, kunyonya na kuwaangusha wasanii makusudi kabisaaa hasa wale WENYE UWEZO MKUBWA WA KUFIKIRI, NK. Halafu wajinga wanapojifanya wa akili zaidi ya mwenye nazo inanikera sana, HAPA NATUMIA MSEMO WA MHESHIMIWA CHG ALIPOMQUOTE SIMKUMBI NANI ALISEMA "inakera sana pale akili ndogo inapotawala akili KUBWA" Sasa hawa clouds na ujinga wao wote eti wao ndio wajanja wa mjini hapa na wanajua kila kitu wakti ni MBUMBUMBU.Hivi kati ya Clouds na Kawambwa anayeharibu wanafunzi na kusababisha matokeo mabaya ni nani manake nawashangaa sana wanaoitisha maandamano kumkomalia Kawambwa ajiuzulu badala ya kudai Clouds ifungiwe kwa kuharibu wanafunzi; eti ooh sijui after school bash, mara ooh bush party, mara ooh mashindano ya vitoto kucheza au kuimba, nk ama kweli nyani haoni kundule.