Nchi yetu inaelekea wapi?

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,970
Tanzania nchi yangu naipenda sana.
Imebidi leo nitoe mawazo yangu kuhusu mstakabali wa nchi yetu hii nzuri sana.
Maelezo haya ninayoyatoa hayaegemei upande wa chama chochote au dini yeyote ni uhalisia wa mambo.

Historia ya nchi yetu na Uchumi wetu.
Wachache hawafahamu kuwa nchi yetu ilikuwa na siasa za ujamaa. Siasa hizi ziliifanya nchi yetu ishindwe kwa namna fulani kujikwamua kiuchumi. Hii ni kwa mantiki kwamba mambo yote yalipelekwa kiujamaa. Isitoshe mwanzilishi wa sela za ujamaaa Baba wa taifa ilifika mahali akachoka.
kwa mujibu wa azimio la Arusha yeye aliye lianzilisha ndiye aliye livunja lilianza vizuri sana lakini lilishindwa kuleta mabadiliko yeyote maana lili feli.

Kuanzia miaka ya 80-90 Tanzania imekuwa ikijaribu kuondokana na mfumo wa kijamaa ili kuingia katika mfumo wa kibepari ambao nchi nyingi zimeendelea kutokana na huo.

Huu mfumo wa kijamaa umewaathiri watanzania wengi, waliowengi kutokuwa na roho ya kuthubutu.

Vile vile Tanzania ilijikita katika kukomboa nchi nyingi za bara la Africa kwa mantiki hii mda mwingi nchi yetu ilitumia kujenga nchi zingine.

Hisia za watu na vuguvugu la kisiasa.
Watu mpaka saa hii wamechoka na mwendo wa maendeleo ya nchi hii. Nchi hii inaonekana inaenda taratibu sana na ikizingatiwa kuwa nchi hii inarasilimali nyingi kuliko nchi yoyote Africa. Hii ninamaanisha haya: Mlima mrefu, Mbuga za wanyama, Mabaki ya watu wa kale, Maziwa makuu, Mito mingi, Aridhi kubwa, Nchi yenye Amani, Nchi haina udini, Nchi haina ukabila, Nchi haina ubaguzi wa langi, Nchi ina bahari na mambo mengi yafananayo na hayo.

Watu wamekuwa wakijiuliza kwanini nchi hii haiendelei? hata mimi pia najiuliza hivyo maendeleo yamekuwa ya taratibu saaaana. Nchi imekuwa ikitegemea misaada kutoka nje kana kwamba sisi watanzania hatuna uwezo.
Mwaka 1992 tulikubaliana kuwa na mfumo wa vyama vingi. Hapa kuwa na mfumo wa vyama vingi ni kushirikiana kujenga nchi hii kwa pamoja.
Lakini sasa kumekuwa na ujinga mkubwa unafanywa na viongozi wa siasa pande zote mbili: Chama tawala na Vyama vya upinzani.

Tumejikita katika marumbano yasio ya tija na yasio na direction yoyote katika maendeleo ya nchi. Naomba wanasiasa sisi watanzania hatutaki umalufu wa mtu sisi tunataka vitu muhimu vizungumzwe na vipatiwe ufumbuzi. haya mambo ya kuanza kusema nani atakuwa raisi ataongoza ni upuuzi mkumbwa.

Sera za nchi na Viongozi wa nchi
Nchi yetu haina sera maalum kwa maendeleo ya nchi. Tumekuwa tukienda tu kama vipofu. Sasa hivi kuna bunge la bajeti hili bunge limekuwa la kukaa na kuongelea matumizi tu ya pesa. Hawaongelei income. Mimi ninavyojua bajeti ni pamija na mapato. Tumejikita katika kuangalia Graph tu. Hizi pesa zinatumikaje hatujui. Mamilioni ya pesa yanatumiwa katika kulipa mishahara, pesa za kujikimu na ruzuku.
Huu ni upuuzi mkubwa kwa nini nchi isiwe na kipaumbele na kukitekeleza? Mnasema mmetenga pesa!? hivi hizo pesa zinatumikaje?

Vilevile viongozi wa nchi wamekuwa wazito sana kuzungumzia mambo yanayojitokeza nchini. Mambo makubwa makubwa yanajitokeza lakini hakuna hata mmoja anayezungumzia. Wamekuwa wanaogopa midaharo ambayo huwa inajenga nchi.

Kwa upande mwingine viongozi wa upinzani wanafanya kinachotakiwa kufanyika. Ila kunawakati wanafanya mambo si kwaajili ya kuendeleza taifa vinaamsha ari kwa wananchi na kuchukia watu fulani fulani(Kuchochea Udini)

Mawazo yangu imefika wakati nchi yetu ikue tuache mambo ya kitoto. Hakuna mtu ambaye hapendi maendeleo ya nchi hii. Viongozi wote wa vyama na Serikali kwanini msikutane na kujadili pamoja mstakabali wa nchi yetu?

Nchi yetu hii itapata maendeleo haraka sana pale viongozi watakapo jitambua. Na maanisha viongozi wa vyama na serikali.

Lakini tukiendelea na matukio ya kijinga kama haya yanayo fanyika:
1. Video ya Rwakatale
2. Mauaji ya waandishi wa habari.
3. Vurugu katika miji mbalmbali.
4. Raisi kusafiri safiri na kukwepa kujibu hoja muhimu.
5. Kutukana vyombo vya ulinzi.
hayo yote na yafananayo nayo ni utoto ifike wakati viongozi waseme basi.


By Annael
Wasalaam



 
Tuungane sote tuijenge Tanzania yetu.
 
yetoni ncho kini iki! tuthitete kana vangondo va ccm vasitete henacho ccm yene hira? ANAEL kuvwinyaje kandu keri keri iti miaka yothe makumi mathano nivo vundu tweenda tuikae huvu? rereha Korea twefanane rae mira uthwi twabaki vakiva ngovori!Vukiva ni ngata?
 

Hatuwezi kuwa wamoja wakati kuna wale ambao kwa sababu ya kuzaliwa MCHAGGA basi haukustahili kuwa MTANZANIA wala haustahili kuwa KIONGOZI wa eneo lolote.

Pili hatuwezi kuwa wamoja kwa kuwa kuna wale wali wanachama wa vyama vya upinzani kwa hiyo wanaonekana ni wapenda madaraka,wadini,magaidi na waleta vita nchini.

Viongozi wetu na wanachama wa CCM wanatakiwa kujua kuwa TANZANIA ni yetu sote bila kajali umetoka dini,dhehebu,kabila au chama pinzani,wakilielewa hilo basi wote watajua na kutimiza wajibu wao.Vinginevyo hali ya kutotoa haki kwa pande zote itakapotamalaki basi tujue fika siyo maskini tu atakayeumia bali hata viongozi na wale wanaofaidi keki ya taifa familia zao,marafiki na ndugu zao pia watakuwa wahanga.

Tuiweke hivi TANZANIA ni yetu sote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…