said:
JF siku zote imekwua ni jambi la kuamsha hisia na kuwa na topic nzito na huu ni mtiiriko kuelekea 2010.Tunahitaji mabadiliko na hatuhitaji kuchoka ili kuendelezea nchi yetu.
Mkuu Gembe, kama ni kweli na wewe umeweza kuliona hili basi ni hatua nzuri na unakaribishwa kuungana na wazalendo kuendeleza libeneke - karibu. Hata hivyo ulichofanya ama unachojaribu kukifanya hakina tofauti na kile tumekuwa tukikihubiri siku zote - kutochoka katika kudai mabadiliko yatakayochochea maendeleo katika nchi yetu.
said:
Mkuu FMES,Mkuu Mwawado na Kada Mpinzani mnahitajika kurudi sasa na kuanza kutoa za changamoto kama za cheche.Watu wamepoa sana hapa JF na tunahitajika kuwa mdomo wa wananchi wa kule tandahimba,uyole na nyarugusu
Inawezekana unaamini kuwa humu ndani wapo watu ambao uwepo wao huleta changamoto zaidi - huo ni mtazamo wako na haki yako. Kwa upande wangu naheshimu mchango wa kuboresha utawala nchini kutoka kwa yeyote bila kutazama majina. Hii tabia ya kujenga matabaka ndiyo yameifikisha nchi hapa ilipo na kamwe tusiiruhusu humu JF.
said:
Tatuzo siyo kulalamika tu,tatizo pia lipo kwenye viongozi tulio nao hasa wale ambao wanapenda 'cheap Politics' bila ya kuwa na sera madhubuti.
Kulalamika ni tabia ya binadamu wakati wowote ule haki inapotolewa kwa kujali sura/wadhifa - usipolalamika ni kuwa unaruhusu hali hiyo iendelee. Sikuelewi unapotumia nano 'cheap politics' na kwa nani. Mtu ambaye amekaa madarakani miaka zaidi ya 30 bila kuleta maendelao, akimwita anayetaka kumwondoa madarakani mroho wa madaraka - hiyo naiita 'cheap politics'. Akitishia kuwa bila yeye amani itatoweka kama vile anayo hatimiliki, hiyo nayo naiita 'cheap politics'. Akibeza sera pinzani na yake ambayo imeshindwa kuboresha maisha ya mwananchi, hiyo pia nitaiita 'cheap politics'. Sasa labda ueleze kinaga ubaga una maana gani na 'cheap politics' na nani unamwongelea hapa.
said:
Tunahitaji kutambua ni viongozi wa aina gania ambao tunawataka kwa hivi sasa,wawe a na sifa gani na hapo hapo tujue tutawapataje?kuwepo na program ndefu ya kupata wagombea ubunge 2010!
Sifa ya viongozi tunaowataka tunazijua na namna ya kuwapata tunafahamu ila tunacholilia ni uhuru na haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Kwa kuwa tunao mfumo wa kidikteta wa chama inakuwa ni vigumu kupatikana utawala unaoheshimu usawa mbele ya sheria. Hivyo njia ziko mbili - kudai mabadiliko katika katiba kwa amani na watawala waone busara ya kuridhia hilo au wawe tayari kusubiri kinachoitwa 'mass action' - shuhudia Thailand !!
said:
Je kwa kutumia vyama vyetu vya siasa au kutengeneza aina ya viongzoi tunawaotaka?wansasiasa ambao watakuwa tayari kupigania maslahi ya nchi yetu bila kuchoka na wenye sera za kimaendeleo! viongozi ambao wanajua kuongoza mambo na kufuatilia kila jambo bila kurukia rukia masuala yasiyo ya msingi.
Wapo wanasiasa tena wengi tu walio tayari kupigania maslahi yetu bila kuchoka - bahati mbaya Mkuu Gembe wewe ni moja wa watu walioshindwa kabisa kuwaona na umeishia kuwabeza wote wanaojitokeza . Umekuwa moja wa watu wanaotetea sera nzuri za CCM ambazo ni wazi hazijaweza kutuletea matumaini yoyote kwa zaidi ya miaka 40 !! If it aint working, fix it and if it cant get fixed, get rid of it, period. Bahati mbaya umebakia kusubiri kumeguka kwa CCM kama njia ya kupata unachoamini upinzani wa kweli - kalaghabaho !!
said:
CHADEMA mlikuwa na Mpango mzuri sana wa kumobilize Vijana ..Umeishia wapi kwa sasa? KWa kifupi tunahitaji viongozi wa kisasa zaidi
Ulianza vizuri sana kwa kuiita hii nchi ya watu kulalamika lakini post yako nzima imejaa kulalamikia wengine tu. Hivi wewe uko upande gani - hebu soma uliyoyaandika:-
said:
Enyi wanachi mlio wakimya,wapole,mlio na uwezo wakushika yale mnayoona ni madogo na kusahu makubwa nawaapieni Kama ukishindwa kuamua
1.Mtaendelea kupuuzwa na kuhudumia wagonjwa!
2.Mtaendela kuishi maisha ya kifukara na kimasikini milele
3.Mtandelea kupuuzwa!
4.Dhahabu na utajiri wote uliopo nchini utachukuliwa na wageni
Tuacheni kuilalamika,tuchukue hatua na kuhakikisha tunaanza upya 2010.
Nawatakieni maandalizi mema na naomba CCM ijetenge ili kufanikisha hili!
Wewe hapa naona umejipanga kama mtazamaji tu - sasa una tofauti gani na hao wanaolalamika. Umesaidia na umeshiriki vipi katika juhudi za kumobilize vijana katika kutafuta uongozi wa kisasa.