Nauza viwanja Ununio

ununio ipo basi haya
basi haya ipo baada ya tegeta na kabla ya bunju.
 
Mh! Mungu anibariki nifungue NGO yangu ya kutetea Haki za wanunuzi wa ardhi,kwa style hii vijana wa BRN walio maliza chuo na kuanza kulipwa laki 3 hawato miliki viwanja.

Mkuu peleka tangazo lako Twitter maana huko ndio kuna mabilionea wanaoweza kununua hivyo viwanja vyako
 
bei ya kawaida sana kwa ununio....kikwete mwenyewe amejengewa nyumba ya kustaafia uko...wewe unataka kuwa jirani na Jakaya kwa kununua kiwanja kwa laki sita sio....
 
Mmh ila ununio ni bado uswahilini sana ni kiwa na maana ukileta ujuaji wazee lazima wakutulize kwa mambo yetu yale ya techonology kuna jamaa yangu kajenga huko sasa hivi anataka kuuza
 
bei ya kawaida sana kwa ununio....kikwete mwenyewe amejengewa nyumba ya kustaafia uko...wewe unataka kuwa jirani na Jakaya kwa kununua kiwanja kwa laki sita sio....

Kwa hiyo kikwete akijenga sehem yeyote bei inapanda...mbona kule msoga haijapanda..acha kuhalalisha wizi
 
Mmh ila ununio ni bado uswahilini sana ni kiwa na maana ukileta ujuaji wazee lazima wakutulize kwa mambo yetu yale ya techonology kuna jamaa yangu kajenga huko sasa hivi anataka kuuza

ununio ipi?
kama ni pale stand kuelekea beach kule kweli ni uswazi (unsurveyed) wanakaa wazawa very local

viwanja vipo upande wa pili wa barabara ya lami kama unaelekea basihaya huku ni surveyed plots only na hakuna mambo ya ajabu kama kule uswazi maana mitaa ya huku kila mtu kajifungia getini.
 


Kweli mkuu kisije kikawa upande pale unaposhukia nyaishozi unakwenda kwa chini yaani kule mwisho kabisa beach kuna soko la samaki alafu akujapimwa watu wamejenga kiholela basi tandale kuna afadhali utafikiri sijui tuko wapi..!
 

Nakubaliana na wewe kwamba hii bei inaweza kuwa kubwa sana kwako lakini kama kweli hicho kiwanja kiko maeneo ya Ununio hasa ile mitaa ya karibu na Beach au barabara ya lami, kumekaa vizuri sana na viwanja ni vikubwa, hakuna uswahili, kumepimwa na kila mtu kajifungia getini kwake. Huduma karibu zote zinapatikana kwa urahisi hasa maji ambayo suala la kukatika hovyo sio kawaida sana. Tena kwa mjasiliamali wa uhakika anaweza tengeneza kitegauchumi cha nguvu na akarudisha hela yake ndani ya muda mfupi sana.

Jambo la msingi, kabla hujafikiria kununua au kubeza hiyo bei fika uione location then argue based on your research evidence. Ni ushauri tu kama mkazi wa maeneo hayo!
 

Ina maana kwa sqr meter 1 = 69,767/=?!

Sasa ukirudi mjini kidogo labda tuseme mbezi beach ungeuza shs. ngapi?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…