Hahahaha me moja nilipewaga kipindi nipo fom six mpaka leo ndo naimalizia fikilia nilienda chuo nkatumia nmemaliza nkatumia nkaingia kazini toka 2013 mpaka leo Yaan nazikubali sana
Hahaha,mie nilipooa basiz ile zanguz oote nikazigawa kwa wadogo zangu,maana wife alikuwa na zake kibao kaja nazo.
Hizo Hapo juu ni za mwaka niliooa 2004,picha hiyo nimezipiga juzi usiku kumjazia mdau,kama mpya.
Ila kama huziju utauzia zenye material siyo,kuna wengine wanafuma kwa kutumia Vitambaa vya mashuka vya Bongo,kama hujui utazukumizwa tu,ila kama umewahi kutumia basi ukiiguza tu unajua kwamba Kitambaa chake ni cha Burundi au Congo original,na kwa mie niliofanya hiyo biashara ndio kabisaa.
Ni sawa na Kitenge cha Wax,Soso au Dubai,uukinipa tu nakuambia ni feki au ni chenyewe.Dar watu wanapigwa saaana hasa kwenye Wax orginal.Ila ndio jiji.
Nataka nikitulia mwakani niangalie baadhi ya Nchi nje ya Tanzania kama zinaweza kupenya kwenye Soko.
Unajua watanzania tunasubiria hadi mgeni aje ndio tuanzishe na sie.
Watalii wengi wanapenda vitu vya kutengeneza kwa mkono na sio Mashine,sasa hizi shuka aisee ukiziangalia unaweza kufikiria mashine,mie miama ya 2000 nilipokuwa nazileta Zanzibar watu wengi walibisha kwamba sio mkono ni mashine.Nilipiga hela ile mbaya,ila niliacha baada ya kuoa hii biashara,maana kwa Wanawake ni balaaa,utavunja ndoa siku sio nyingi.
Wife alipokuja akaanza kiasi then watu wakawa wagum saana kulipa,tuka quite
Ila akitokea mjanja akaanzisha hii biashara kisasa zaidi itamlipa,ila lazima ajue kutoka kwenye soko la nje ya nchi,asihofie ushindani wa shuka za viwandani,huku Zanzibar watu wananunua mavitu ya ajabu bei kubwa kweli na wakati vya viwandani vipo,kazi za mkono wenzetu wanazihusudu saaana,tena uzuri wa shuka hizi mie nilikuwa napiha hela ile mbaya kwakuwa nilikuwa na deal na maharusi saaana,nachukua Order then namuambia mfumaji kwamba fuma jina la maharusi.Basi ukiwapelekea aisee wanafurahi sana unakula tenda tena.Maana order maalum ya Mfumo wa mjazo inaweza kufika mwezi mmoja mpaka miwili kuifuma inategemea na aina ya Copy yenyewe.Na rangi zenye kutoka sana ni Nyeupe,maroon na Zambarau
Ilikuwa wastan wa shuka 20 kwa wiki naagiza na zinaisha zote.
Mjanja aanze na website then ahakikishe anakuwa na aina zote za nguvu,apenye soko la nje.Mtaji wake ni wakawaida sana.Mwaka 2000 ilikuwa Tsh: 12,000 kwa jumla,ambapo mie nilikuwa nauza 25,000
Majuzi tu kuna family friend walitaka wife awasaidie kwa kumuomba saana, kwa ajili ya Harusi,akafuma mwenyewe akalamba 75,000.Wakali gharama halisi za Nyuzi na Shuka plain haikuzidi 25,000.
Ukizoe shuka hizi sio siri,kama teja unakuwa,yaani haya mashuka ya madukani hununui,mie mpaka leo sijui shuka hizi za madukani za kupack ni bei gani.All my shukaz ni kama hizo.
Mjanja aanzishe