1. Nijuvye mpenzi wangu, hali yako ulonayo
Zimepita siku chungu, sijasikiya haliyo
Hukaribu chini yangu, nikapoza huu moyo
Naungulika kwa hayo
2. Waniruka usingizi, kucha nikikufikiri
Hebu itika azizi, iondowe yako ari
Siku naiona mwezi, kwako sina ujabari
Naiogopa kwaheri
3. Kama uko ugonjwani, nambie nije haraka
Nitafute chombo pwani, au ndege ntaruka
Nifike kwako ayuni, roho itafurahika
Niondowe yangu shaka
4. Lau kama nimekosa, nikheri uniambie
Hivi sasa wanitesa, dhiki naijuwa mie
Sina moja la anasa, nimekonda kama sie
Mwenzio nihurumie .