habarini wanajamvi, Nina Mahindi yangu nililima Morogoro na mengine nimeongezea hukuhuku kwa wakulima hivyo nimefikisha gunia 500,naomba kujua bei yake Kariakoo au mwenye shauri niuze wapi kwasababu nilikua nategemea kuyauza Kenya sasa wenye magari wanagoma wanadai kuna folen Sanaa hivyo magar yanachukua wiki nne hadi kushusha inakua hasara kwao msaada tafadhari,nawasilisha,Mimi nipo Morogoro
barikiweni
Sikiliza Radio One kila siku asubuhi wana bei za masoko mbalimbali. Ukishapata bei ya jumla sokoni utaweza kupima ujuwe kama ukiyasafirisha mpaka Dar itakulipa au itakuliza.
Mkuu blessingskd jaribu kucheki na watu wa kanda ya ziwa, inasemekana bei ni nzuri huko. Ili upate faida kubwa chukua semi lenye uwezo wa kubeba gunia 300 at par. Debe kule Sengerema ni sh12000, so sio mbaya kama utauza kila roba kwa sh70,000*300=21M na cost ya kupeleka mzigo haizidi 3M.
Then ukirudi unaongezea mzigo wa gunia 100 ili zitimie 300. Vijiji vya wilaya ya Kilindi mahindi sahz ni sh3000 kwa debe. Gunia 100=tsh 2.1M
Kazi kwako mkuu!
kua makini na soko la mahindi mwaka huu! changamka mapema kwani karibu kila sehemu tz wamevuna vizuri(kilimo kwanza?) alie zungumzia kanda ya ziwa si kweli, debe halizidi 7000.
kua makini na soko la mahindi mwaka huu! changamka mapema kwani karibu kila sehemu tz wamevuna vizuri(kilimo kwanza?) alie zungumzia kanda ya ziwa si kweli, debe halizidi 7000.