Natafuta Mtaji

Hypasonic

Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
14
Reaction score
6
Ndugu wananchi wenzangu Habari zenu!!
Kwa juhudi nilizozifanya mpaka sasa hazijazaa matumaini kabisa (kwa kipindi cha mwaka mzima mpaka sasa), nahitaji mtaji wa kiasi cha shilingi milioni 400. Je kiasi hichi nataka kufanyia nini?

Uanzishwaji wa Chuo cha Afya katika wilaya ya Mpwapa Mkoani Dodoma.

Chuo cha ngazi gani?
Uwekezaji wangu ni wa chuo cha kati (mid-level health college), vyuo hivi hutoa mafunzo ya wataalamu wa kati ama (technical education) na hutoa wataaluma kwa upande wa afya hutambulika kama kada ya kati ama (mid-level health professionals). Mafunzo chini ya vyuo hivi hutoa uhitimu kwa ngazi ya cheti mpaka diploma (mitaala ya masomo ya afya kwa mfumo wa uhitimu huo yapo kuanzia NTL level 1 mpaka level 6, level 1-4 ni masomo ya cheti na level 5 na 6 ni masomo ya diploma) mbali na mitaala hiyo pia kuna mitaala kwa fani maalumu. Vyuo vya ngazi hii husimamiwa na NACTE kama taasisi na husimamiwa pia na mabaraza ya taaluma ya afya kwa maana ya utoaji mafunzo na uendelezaji mitaala (mfano, nurse, clinical medicine, Pharmacy, Medical laboratory, environmental health science etc).

Kwanini niwekeze kwenye mradi huu?
Kama mwananchi kuna fursa nyingi za kulisaidia Taifa na jamii kwa ujumla. Mahitaji ya wafanyakazi kwa sekta ya afya ni nusu ya wafanyakazi wote waliopo sasa kazini, hasa kwa wafanyakazi wa kada ya kati na hii ni kwa watoa huduma wote, Public, Private na FBO. kuna mapungufu mengi sana katika vyuo vya afya vya ngazi hii, hasa upande wa walimu na vifaa vya kutolea mafunzo, mazingira ya wanafunzi na utaratibu mzima wa mahusiano ya kitaasisi. Tanzania wenye sifa za kuingia mafunzo ya masomo haya ni wengi lakini nafasi ni chache, na wengi hawana taarifa sahihi juu ya vyuo na uwezo wake. vyuo vingi vya ngazi hii ni vya serikali, mpaka leo maudhui ya kuanzishwa kwao kwa vyuo hivyo hayajabadilika hivyo ni vigumu kupanuka na kuchukua idadi kubwa ya wanafunzi (maudhui ya vyuo vingi vya ngazi hii kwa upande wa serikali ambavyo ni asilimia 80 ya vyuo vyote vilivyopo vya ngazi hii ilikuwa ni in-service training, kuendeleza mafunzo kwa wafanyakazi waliopo hospitalini wameajiliwa tayari, hivyo miaka ya karibuni baada ya kuona mahitaji yanazidi kuwa makubwa na wafanyakazi wengi wa afaya tayari kuna tatizo la umri, wakabadilisha utaratibu na hivyo kuanza kutoa pre-service training maana yake watu ambao hawana elimu ya taaluma za afya kabisa. kwahiyo no link between production and actual national deficit, mpaka leo hakuna National strategy ya human resource development katika wizara ya afya inayo link uzalishaji (production and national requirement kwa kada za kati) na mahitaji ya kitaifa.

Upatikanaji wa wanafunzi
kulingana na uzoefu nilionao kwenye programu mbalimbali za rasilimali watu kwenye sekta ya afya, kuhusu upatikanaji wa wanafunzi sio tatizo, kwani nime apply, mechanism ya Bonding and Sponsoring kwa wanafunzi wanaotoka maeneo ya vijijini (target ni mikoa ya kati na kanda ya ziwa) kwa wale wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na wanasifa ya kujiunga hata kidato cha sita wanaingizwa katika mpango huu ambapo watalipiwa gharama zote za masomo pamoja na accomodation kwa kipindi chote cha masomo yake, na mara baada ya kumaliza watatakiwa kurudi kufanya kazi maeneo waliyotoka kwa angalau kipindi kisichopungua miaka mitatu, mpango huu utafadhili watoto 250, na tayari mashirika kadhaa na makampuni yanayoendesha shughuri zake wilaya zilizo na uhaba wa wafanyakazi zimekubali kushirikiana. Pili kuna shirika lisilo la kiserikali linalotarajia kuanza kazi zake za kuhamasisha wanafunzi wa sekondari kuzingatia masomo ya sayansi, ikiwa malengo ni kuongeza idadi ya wanafunzi wenye sifa za kujiunga na masomo ya afya kwani ukweli idadi inashuka sana ndiyo maana wanaopatikana wanatoka mweneo mbalimbali huwezi kupata wanafunzi idadi kubwa toka sehemu moja. Mbali na mipango hiyo pia tutatumia utaratibu wa kimasoko na teknolojia kuwafikia wengi kama nilivyojipanga.
Suala la ada
Ni angalizo ambapo wengi wanaosimamia vyuo vya afya sio wanataaluma ya uendelezaji wa taasisi hizo hivyo wanakosa ubunifu wa vyanzo vya mapato na kuishia kutumia tozo za ada kama chanzo kikuu cha kupata fedha za kuendeshea mafunzo na huduma nyinginezo, jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa ada kusikolingana na huduma zenyewe (Value of money). chuo kimetenganisha, College core business na other business (core ni utoaji eleimu) masuala mengine yote ni huduma nyinginezo ambazo na hivyo chuo kiwe na running cost ndogo kwa kuhakikisha huduma nyinginezo zina link na kampuni rafiki ili kupunguza gharama za kuwa na wafanyakazi wengi na hata ghalama nyinginezo zinazotokana na uendeshaji huduma, na pia kutenganisha kila huduma ikawa inajitegemea na hivyo kuleta profiti zaidi.

Nini nimefanya mpaka sasa?
Baada ya kuachana na habari ya kuajiliwa bada ya miaka kumi ya ufanyaji kazi katika sekta ya afya. nikiwa mmoja wa waandaaji wa National PPP policy and Act, nilijitolea kufanya kazi na watu, mashirika ya ndani kwa kuboresha vyuo na mambo yanayohusiana na usimamizi wa vyuo vya afya nchini. mwaka jana kuanzia mwezi wa kumi nikaamua sasa kushughulikia mradi wangu huu, baada ya kufanya upembuzi wa kina nikachagua kanda ya kati kuwekeza mradi wangu na maalumu kabisa mpwapwa kutokana na historia ya mji huo kwa mazingira ya utoaji elimu tokea enzi za mjerumani kabla ya mwingireza kuja na mradi wa mashamba ya karanga. lakini mradi wangu unahitaji mambo mengi ikiwa majengo ya kutosha kwa idadi ya chini ya wanafunzi 900 kwa fani mbalimbali. uwezo wa kujenga majengo sina, nafanyaje? hivyo ilinibidi kuangalia fursa zilizopo na namna ninavyoweza kutumia hasa kwa majengo ya taasisi mbalimbali yaliyopo wilayani pale. Hatimaye nikapata kuyaona majengo na eneo kubwa la Chuo cha ufundi, kwa wale wenye umri mkubwa na wengine waliosoma mpwapwa watakuwa wanajua majengo na eneo la chuo cha ufundi cha Magogo mpwapwa. Hiki chuo kinamilikiwa na Roman Catholic jimbo la Dodoma, lakini tokea miaka ya 2000 mafunzo yalisimama na hivyo veta walikuwa wakitumia majengo hayo kwa kuwafundishia wanafunzi wao na kama kituo cha mitihani. Hivyo nikaenda kuwaona wahusika wa eneo hilo na baada ya kukaribishwa nikaomba kufanya upembuzi kama nikihitaji mejengo yale kwa vigezo vya chuo cha afya nini kitanighalimu na kwa kiasi gani, baada ya kujiridhisha kwa timu ya mafundi mbalimbali kufanya upembuzi wa kimahitaji (renovation and construction) nikaonatoa uamuzi wa kuonana na uongozi wa jimbo na kuomba kupang majengo hayo na eneo lile. Hatimaye baada ya kufikisha maombi na kuitwa katika kikao cha bodi ya wadhamini wa jimbo tukazungumza vyema na common goals zikaanishwa hatimaye tarehe 30 mwezi wa nne mwaka huu nikapata kukubaliwa kupanga majengo hayo na eneo lile kwa kipindi cha miaka 5 baada ya kufanya ukarabati na kusajili wanafunzi, makubaliano yameweka wazi mkataba nilionao ni renewable contract ambapo bada ya kipindi hicho cha awali tutafanya review na kama itafaa basi tutaingia ubia, roman na mimi kuendesha huduma ya utoaji mafunzo kwa kuwa we have common goal to serve community, but making profit too.
Tokea mwezi wa nne nimetafuta funds hata milioni 100 za kuanzia sijafanikiwa.
Muda wa kuanza mafunzo:
kama nikipata mtaji kwa sasa, maanayake ukarabati utaanza mwezi wa tisa na hatimaye usajili wa chuo utakuwa by december na usaili wa wanafunzi utafanyika intake ya march 2015. lakini kuna baadhi ya mafunzo yataanza hata kabla ya usajili kwani mafunzo hayo yanahitaji uwepo wa lab skills na vifaa vya kufundishia.

Uzoefu katika masuala ya afya:
Health system management by professional, nimefanya kazi kama technical advisor mashirika ya kimataifa, kwenye umoja wa mashirika ya wahisani katika sekta ya afya, kwenye national steering team na Task force za wizara ya afya kwa miaka mitano, na incharge wa masuala ya human resource development for health sector kwa mikoa mine, Lindi, mtwara, Tanga na mbeya. pia mshauri wa uendeshaji na usimamizi wa vyuo vya afya vya kada ya kati kupiti Zonal health resource centre za wizara ya afya.

Mwisho
Nitashukuru kupata ushauri wenu wananchi wenzangu, pesa si ninachokitafuta pekee, maoni yenu yanathamani kubwa sana katika ulimwengu tuishio sasa.







 
hii ndio tz, watu wanataka waone umeanza mwenyewe kwanza,ndio wakusapoti
 
hii ndio tz, watu wanataka waone umeanza mwenyewe kwanza,ndio wakusapoti

Mwenzio akianza kuwekeza wewe unakuja kusapoti nini? Naunga mkono kauli yako kwani wengi hujifanya hawaoni juhudi za watu wengine, lakini ukisha fanikisha basi hao, wanamiminika. ninawashangaa sana watu wa benki, ukiwa na juhudi za kuanza kuwekeza wanakaa mbali, ukianza wanakuja kutaka kutoa huduma za kibenki kwa taasisi husika, mara wanafunzi wafungue akaunti kwetu...jamanii.... Tanzania ni zaidi ya nchi ya kufikirika
 

ndio hivyo mkuu. busines plan zinadharaulika sana bongo..
 
Nina vyanzo vya taarifa za mashirika ya wafadhili wa miradi.Nitafute via educationalngos@yahoo.co.uk

hivyo vyanzo vya taarifa za mashirika ya wafadhili wa miradi kwa nini usiweke hapa jamvini tukashare na wadau wengine?
 
Asanteni wadau kwa maoni na michango yenu...mnajua katika nchi yetu hakuna chuo cha afya ya kati chenye maabara ya vitendo..(lab skills) kama inavyohitajika, zaidi ya kuwa na midoli miwili na skeletoni za kufundishia, yaani concentration ya vifaa vingi vilivyopo ni vya Anatomy and Physiology. Bila uwepo wa lab skills zenye vifaa muhimu ..Competence Based Teaching Methodology ni ngumu sana jumlisha mabadiliko ya mitaala ya afya kwa kada za kati ya mwaka 2009 uwezo wa wahitimu kwa asilimia kubwa ni wa kiwango cha chini kwani hata mahosipitalini wanakotakiwa kufanyia mazoezi kuna changamoto nyingi ikiwa Clinical mentors kwa vyuo husika hawapo na hivyo kusababisha wanafunzi kupata nafasi chache sana za kuelimishwa ipasavyo maeneo mbalimbali wanayohitaji kujifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…