Uko sahihi ndugu yangu. Tulikosea mwanzoni tulipo rudisha nchi yetu katika mfumo wa vyama vingi, Ingawa viongozi wa chama tawala wa wakati huo walikubali mfumo wa vyama vingi urudi, lakini walitumia nguvu nyingi sana kuupaka kinyesi na kuwaaminisha wananchi kuwa vyama vya upinzani ni chanzo cha machafuko wakitolea mfano Mauaji ya Rwanda.
Kutokana na hayo na kukosekana kwa elimu sahihi ya faida kubwa ya vyama vingi kwa maendeleo ya nchi imesababisha vyama vyote nchini kikiwemo CCM chenyewe kuacha misingi yao na kuendeshwa kwa maslahi ya Viongozi wa vyama hivyo badala ya kuangalia maslahi ya Taifa kwa ujumla (Ubinafsi, chuki za kijinga, Visasi, na ubadhilifu)
Kwakuwa wananchi wa kawaida tumekosa msingi mzuri wa siasa za vyama vingi, tumejikuta tuna bobea katika ushabiki wa vyama (Ukereketwa na ufurukutwa) bila ya kujali kama viongozi wa vyama wana simamia maslahi yetu kama katiba ya vyama vyao zinavyo hubiri ama wana tupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Pamoja yakuwa nchi yetu tumekuwa tuki jinasib kuwa hakuna ukabila na udini (Ingawa kwamtazamo wangu naona hayo mambo yote yapo nchini ingawa kwa kiwango kidogo ukilinganisha na nchi jirani) Tuna tatizo kubwa sana la kuabudu vyama vyetu na viongozi wake, kiasi cha kufumbia macho mapungufu na kutetea mapungufu ya wazi kabisa na hata kutamani kuua watanzania wenzetu ili tutetea maslahi ya vyama na viongozi wetu bila kuangalia UTU na UTAIFA wetu. Ubaguzi na ukandamizaji unao onekana katika UDINI, UKABILA na UKANDA katika nchi za wenzetu kwetu sisi umebebwa kwa kiasi kikubwa na UVYAMA.
Sitashangaa kama sikumoja nchi yetu itangundulika kuwa ni nchi inayo ongozwa na Kabila Moja!!!, Dini Moja!!! Ukanda mmoja uitwao !!!!πππ