Katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Nape kapingana na katibu wake ambaye hapo awali alidai kuwa wanaitisha kikao cha dharura kuijadili rasimu ya katiba mpya kwa maana hawajakubaliana nayo kama chama. Lakini Nape kadai yeye alishasema kuwa anakubaliana na rasimu hiyo na alishawapongeza kina Jaji Warioba kamalizia kuwa hayo maneno ya kutokubaliana nayo ni ya mitaani kwa vile yeye ndo msemaji wa chama chao.
Source: BBC
--------------------- Ufafanuzi wa Ndg Nape Nnauye.