Jambo la kwanza ambalo mimi ningekushauri ufanye ni kuvunja ukimya na kuongea na mwenzi wako juu ya swala hili. Mweleze ni jinsi gani unakereka na jambo hili na namna ambavyo ungependa awe, kama kweli anakupenda atakusikiliza na atabadilika na kama asipobadilika basi ujue huyo hakufai. She is not your type.
Ndiyo tabia za hivi viumbe. Kubebwabebwa tu. Hata mawaziri wanawake ndiyo zao hizo kwa wanaume wao. Huna jinsi mvumilie tu.Nina mchumba wangu tunaishi sehemu tofauti tena mbali. Kuna tabia anaifanya sivutiwi nayo. Hii tabia ni ya kunibeep, kutuma tafadhali nipigie au naomba niongeze salio. Hii imekuwa ikijitokeza mara nyingi mpaka nafikia kukereka moyoni. Huwa nampigia mara nyingi kwa siku tunaongea na huwa namwongezea salio pale ninapokuwa nazo. Lakini mwenzangu muda wowote atatuma tafadhali nipigie au naomba niongeze salio. Kwa kweli nachukizwa na hii tabia ila kumwambia naona kama ataudhika na kuanza kutofautiana. Nampenda sana na nimeshamtambulisha home. Huko nyuma kuna binti niliwahi kuachana naye sababu ya mambo haya. Ulikuwa ukimtumia salio hakupigii ila anakubeep na kutuma tafadhali nipigie,nilimwelimisha lakini hakubadilika. Nikahisi ni utoto hivyo bora nimuache na watoto wenzie(alikuwa first yr chuo). Sasa huyu ni mfanyakazi bado ni yale yale. Hivi wadada wote mko hivi? Nitafanyaje ili nimfikishie ujumbe bila kuvuruga uhusiano wetu? Nampenda sana,nahisi hii kitu itatuvuruga.
Mimi ni mwanamke kwa upande wangu kabla hatujaoana sikupenda kabisa hy mambo ambayo mchumba wako anakufanyia! Ina maana yeye huwa anampigia nani km unampa vocha na bado anakubip? Wanawake wa staili hii ni hatari sn, hata mliwa kwenye ndoa, usitegeemee mshahara wake kusaidi mahitaji hom, utawajibika kwa kila kitu. Utakuta hata ukipanda daladala hawezi lipa npk we ulipe. Mchumba anayefaa hawezi kuluchuna vocha kihivyo kwanza huwa ana uchungu na pesa yako. Kaa chonjo utaishia kuhonga usipokuwa makini!
Nipe namba yako nikupunguzie salio wewe na mpenzi wako.
haya mambo ya simu za mkononi yame-complicate sana maisha...; mahusiano yanavunjika, watu wanakufa, yaani balaa tupu
usipoziba ufa utajenga ukuta,navojua mimi mapenzi nimawasiliano ikiwa nipamoja nakuambizana ukweli hatakama unuma mwambie unavojickia nayeye anatakiwa akuelewe vingnevyo mbele yasafari utashindwa kukemea makosa mengne makubwa kisa unaogopa atachukia.