Naomba kujua historia ya Urusi

Nimesabcrib huu uzi sas milivyoona notification ya Emperor mbio mbio nimefungua. Hope umesema sio mda mrefu...
Wengine masomo yetu yalikuwa ya catalyst so ninaposoma post zako juu ya hii mada napata urahisi wa kuelewa dunia ilivyokuwa na ilivyo.

Nashukuru sana mkuu, tupo pamoja.

Na mimi nakusubili kwa hamu The Emperor kwa hatua zinazofuata!!

Karibu sana mkuu
 
Nice history
 
Asante mkuu mimi nilitaka kujua ilikuwaje Urusi pamoja na uwezo wake mkubwa wa Kijeshi akashindwa huko Afghanistan,na pia Marekani kushindwa huko Vietnam
Mkuu napenda kuongezea swali kuhusu Vita ya USSR vs Finland maarufu kwa jina la "The winter war" iliyotokea 30 November 1939 hadi 13 March 1940. USSR ilishindwa vibaya na kainchi kadogo ka Finland huku vigogo na wakuu wa kisoviet kama Nikita Khrushchev na Joseph Stalin aka The man of Steel aka Koba wakishikwa pabaya na Finland

Kwenye Historia ya Urusi hiki kipande hakijaguswa. Wakuu hebu tupieni hoja hapa inakuwaje Finland kuichapa USSR? wakati USSR ameweza kuichapa NAZI Germany kwenye ile operation maarufu ya Hitler kuivamia USSR maarufu kwa jina la "Operation Barbarossa"?
 
Nadhani Kabaunyeri na The emperor watatusaidia kwa hili maana liko ndani ya uwezo wao.
 
Nilichojifunza kuhusu warusi waliwekeza zaidi kwenye teknolojia ndio maana wapo powerful.wana kila aina ya teknolojia unayoijua na usiyoijua wanaitengeza wenyewe sisi tuna import technology for use only

Kuwekeza kwenye Elimu kuna matokeo chanya kwa kila taifa hapa duniani. Mitaala ya Elimu ya nchi za Marekani na Japan kuanzia mwaka 1985 iliiga ule wa Urusi kwasababu ulikuwa umejaa elimu kwa vitendo na unamjenga sana mwanafunzi kitaaluma hasa kwenye masomo ya sayansi kwa vitendo.
 
kama viongozi wetu wangekua wanazingatia ushauri wa hapa JamiiForums tayari tungeanza kuvuna wataalam wabobezi katika elimu ya sayansi kwa vitendo mbali na sayansi ya siasa!@THEEMPEROR endelea kutupa nondo
 
hapo viongozi hasa sekta ya elimu waache kuhubiri majukwaani maswala ya elimu bali waboreshe mtaala ili kuendana na dunia ya sasa,hapo tutajenga taifa imara tukiamua kuwekeza katika elimu ya vitendo,emperor usisahau kushusha nondo kuhusu historia ya urusi hasa pale walipowadhibiti USA walipotaka kumpindua Castro na majaribio zaidi ya 600 ya kutaka kumuua Castro lakini wakashindwa
 
Tanzania tukijipanga vizuri tutaweza kufanya vizuri sana kijesshi, kiuchumi, kijamii nakisiasa duniani
Tatizo letu hatuna sera ya kitaifa, tuna maslahi ya vyama wala sio nchi.
Ka

Laiti kama tungekuwa na hii kitu, tungekuwa mbali. Bila kujali chama, yaani aje CDM au ccm, sera ibaki pale pale nchi na malengo yetu na mwelekeo wetu kama taifa tungekuwa mbali mno.
Kwa sasa ni ngumu, angalia ccm wako tayari kutumia vyombo vya nchi kuangamiza upinzani, kwa mwendo huu hatuwezi kupiga hatua.
 
I wish I could be The Emperor
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…